'Alimpoteza mama yake wakati wa kuzaliwa,'Ababu Namwamba aeleza yaliyomtokea bintiye

Muhtasari
  • Ababu Namwamba aeleza yaliyomtokea bintiye
Image: Ababu Namwamba/TWITTER

Aliyekuwa Mbunge wa Bundalangi Ababu Namwanba amewapa Wakenya maelezo mafupi kuhusu kisa cha bintiye mkubwa aliyetambulika kwa jina la Esther.

Akishiriki picha nzuri ya familia yake wakitembea kwa mbwembwe chini ya hali tulivu ya Kijiji kilicho karibu cha Budokomi kilichowekwa katikati mwa eneo la Matayos katika Kaunti ya Busia, Ababu Namwamba alikariri yaliyomtokea mrembo Esther miaka 5 iliyopita.

Namwamba alieleza kuwa Esther alimpoteza mamake mwaka wa 2016 wakati wa kuzaliwa. Katika juhudi za kuweka nyota yake mrembo kung’ara, Namwamba aliamua kumchukua Esther kuwa bintiye huku akimlaza mamake.

Namwamba amesisitiza kwamba amekuwa babake Esther tangu 2016 na babake mzazi amekuwa kaka yake tangu wakati huo.

"Jioni njema nikiwa na binti yangu maalum, Malkia Esther katika Kijiji cha Budokomi Matayos Busia. Esther ni muujiza mpendwa

Alimpoteza mama yake wakati wa kuzaliwa miaka 5 iliyopita. Tulipomlaza mamake mwaka wa 2016, nikawa babake Esther. Baba yake Martin amekuwa kaka yangu tangu wakati huo," Aliandika Namwamba.