Nataka mwanaume tajiri, wanaume maskini hufikiri kuhusu ngono tu - Justina Syokau

Muhtasari

•Syokau alisema anatafuta mwanamume tajiri, anayewajibika  na ambaye hawatazozana sana naye watakapokuwa kwenye ndoa.

•Alifichua kwamba aliteseka sana katika ndoa yake ya kwanza hadi akaamua kugura miaka tisa iliyopita.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau almaarufu kama 'twedi twedi' amekiri kwamba sasa amechoka kuwa pwekee na  anatafuta mchumba.

Akiwa kwenye mahojiano na Eve Mungai, Syokau alisema anatafuta mwanamume tajiri, anayewajibika  na ambaye hawatazozana sana naye watakapokuwa kwenye ndoa.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema anawaepuka wanaume fukara kwani anahisi kama kwamba mara nyingi wao hufikiria tu kushiriki tendo la ndoa badala ya kuwajibika.

"Moto upo. Mtu atakayenipenda nitalia. Nataka tu kulilishwa na mapenzi, sitaki kulilishwa na vurugu. Nataka mwanaume tajiri anayewezana na maisha. Hatutakuwa na misukosuko mingi na mwanaume tajiri, lakini wanaume hawana pesa tutasumbuana sana nao. Wanaume maskini hufikiri kuhusu ngono tu, huwa hawana bidii ya kufikiria kipi kingine. Nataka mwanaume ambaye  ambaye anafikiria kuhusu kuwekeza, mwanaume anayewajibika ambaye tutaweza kulisha watoto naye. Sio mwanaume ambaye ananiacha niwajibike mwenyewe" Syokau alisema.

Mwanamuziki huyo alifichua kwamba aliteseka sana katika ndoa yake ya kwanza hadi akaamua kugura miaka tisa iliyopita.

Amekiri kwamba tangu alipotengana na mumewe amekaa bila mchumba na hata hakuna ambaye amekuwa akionja tunda lake.

"Nimekuwa pekee yangu kwa miaka tisa. Nilikuwa nimeolewa kisha tukatengana na mume wangu. Nilisema ni vizuri nipumzike kidogo ili nilee mtoto kwanza. Mtoto wangu ana miaka tisa sasa. Corona ilifanya hisia zangu zirudi. Nilikaa kwa nyumba hisia zikaanza kurudi" Alisema Justina.

Justina alisisitiza kwamba anammezea sana mwanamuziki mwenzake Ringtone Apoko na angetamani kuwa mke wake.

Alikiri kwamba Ringtone akaamua kumchumbia sasa hawezi kusita kukubali ndoa naye kwani anaamini kuwa yeye ni mwanaume mzuri.