'Acha nikae kimya!'Mulamwah asema baada ya drama yake na mama wa mtoto wake

Muhtasari
  • Mulamwah alidokeza kuwa suala hilo ndilo lilichangia kutengana kwao takriban miezi sita kabla ya mtoto kuzaliwa
Mulamwah
Image: Facebook

Mapema wiki hii mcheshi Mulamwah na mama wa mtoto wake Carol Sonnie walianza kuanikana mitandaoni, huku Mulamwaha akitoa sababu kuu ya kuachana naye.

Mulamwah alidokeza kuwa suala hilo ndilo lilichangia kutengana kwao takriban miezi sita kabla ya mtoto kuzaliwa.

"Huyo mtoto mnaona akibebwa na kupigwa picha saa hizi, mnajua mamake alikuwa amemtoa kweli? Akiwa na ujauzito wa miezi mitatu alikuwa ashameza tembe, mtoto alikuwa anatoka. Mimi niligundua kuchelewa kuwa alikuwa anafanya hivo. Nilienda hospitali nikatumia pesa sijui ngapi kuhifadhi ujauzito huo" Mulamwah alidai.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa amelazimika kuvunja kimya kuhusu yaliyotokea baada kuona mzazi mwenzake bado analizungumzia suala hilo.

"Msidhani mambo yanatendeka hivo tu. Kuna sababu za kila kitu. Tukiamua kuongea maisha ya watu itaharibika huku nje. Stori ni mingi. Mambo yanaharibika. Tunajaribu kunyamaza na kutoa watu mitandaoni na hawasikii" Amesema.

Carrol Sonnie kwa upande wake alisema anachagua kusalia kimya licha ya yote yanayosemwa dhidi yake.

"Kwa heshima niliyo nayo kwa Keila na kwangu mwenyewe, , bado nachagua kusalia kimya" Sonnie alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Pia Mulamwah baada ya kulipua hayo yote alipakia kibao chake Diamond kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kwamba acha akae kimya baada ya yote.

Je kulingana na maoni yako wasanii, watu mashuhuri wanapaswa kuanikana mitandaoni baada yao kukosana?