Mtunzi na mwimbaji wa Uingereza Ed Sheeran anaendelea kuongoza kwenye chati za muziki si tu nchini Uingereza bali dunia nzima kwa weledi wake katika kutunga mashairi yenye vina vya tafsiri.
Hii ni baada ya ngoma yake single ya ‘Shape of You’ kutangazwa kuafikia kiwango cha juu Zaidi cha 9X platinum nchini Uingereza.
Single hiyo ambayo aliitoa mwaka mwa 2017 ilipata mapokezi makubwa kote duniani ambapo iliongozwa chati za miziki nchini Uingereza kwa wiki za kwanza kumi na nne mtawalia na kitengo cha ngoma single.
Katika kipindi hicho cha siku kumi na nne, ‘Shape of You’ ilipata streams milioni 224 na kupakuliwa mara 765,000, rekodi ambayo iliandikishwa upya na kufanya ngoma hiyo kutunukiwa kiwango cha 5X Platnum katika mwaka huo wa 2017 na baadae album ya ‘Divide’, ilimotoka ngoma hiyo kutunukiwa kiwango cha 7X Platnum.
Wakitangaza kiwango kipya cha 9X Platnum ambacho single hiyo ilifika, rekodi lebo na wasambazaji wa muziki wa Uingereza, British Phonography Industry, BPI walisema kwamba ‘Shape of You’ imekuwa kama wimbo wa taifa kwa kizazi cha sasa na ni hit ambayo itasalia kushabikiwa kwa miaka mingi ijayo.
BPI ambao pia ndio wandaaji wqa tuzo za BRIT Awards ambazo zinatangaza washindi hao walisema kwamba sasa ngoma hiyo ya Ed Sheeran imedhibitishwa kuwa BRIT 9X Platnum. Katika tuzo hizo, ngoma hiyo ilitajwa kuwa bora kwa karene hii.