Mike Sonko awaomboleza wazazi wake huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Mike Sonko awaomboleza wazazi wake huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa
Mike Sonko
Image: Facebook

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Mfanyabiashara huyo mahiri alienda kwenye mitandao yake ya kijamii kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuwaenzi wazazi wake.

Sonko aliwashukuru wazazi wake, na kuahidi kamwe hatawaangusha.

Alitaja kwamba walipitia magumu mengi kumlea. Babake Sonko Gideon Kioko Kivanguli alifariki katika Hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mfupi miaka sita iliyopita.

Mamake Sonko Saumu Mukami Mbuvi aliaga dunia mwaka wa 1997.

"Licha ya dhiki zangu ninastahili kuwa na furaha kama Mkenya mwingine yeyote. Leo ni siku yangu ya kuzaliwa na napenda tu kumshukuru Mungu kwa kuniongezea mwaka mwingine katika maisha yangu. Nitakushukuru daima, Mungu.

Pia ningependa kuwashukuru marehemu wazazi wangu wanapoendelea kupumzika kwa amani kwa kunileta dunia hii, Mama na Baba… mlipitia magumu na maumivu mengi.

Lakini ninaahidi, sitaacha yote hayo yaende bure. Ninataka kutenda haki kwa kila wakati uliniamini. Kwa watu wangu ungana nami katika kujitakia siku njema ya kuzaliwa. Mimi penda nyinyi sana.."