Mungu wetu ni wa upendo-Rose Muhando amtakia Professor Jay afueni ya haraka

Muhtasari
  • Nyota wa nyimbo za injili Rose Muhando, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemtakia Jay afueni ya haraka
Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Image: HISANI

Nyota wa muziki kutoka Tanzania Joseph Leonard Haule almaarufu kama Professor Jay anaendelea kupokea matibabu maalum katika hospitali ya Muhumbili baada ya kushikwa na a na maradhi wiki kadhaa zilizopita.

Taarifa kutoka Bongo zinasema kuwa rapa huyo ambaye amekuwa akitumbuiza kwa miaka mingi na pia kuhudumu kama mbunge alilazwa takriban wiki tatu zilizopita akiwa hali mahututi.

Wiki chache zilizopita Familia na marafiki wa Jay sasa walitoa wito wa msaada wa kifedha kutoka kwa wasamaria wema ili kugharamia matibabu yake.

Nyota wa nyimbo za injili Rose Muhando, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemtakia Jay afueni ya haraka.

Hata hivyo msanii huyo alimweleza kwamba mika miwili iliyopita alipitia aliyoyapitia, lakini Mungu alikuwa mwaminifu kwake kwani ni Mungu wa upendo.

Pia Rose alitoa mfano wa Ayubu ambaye alijaribiwa na magonjwa na kudao kwamba magonjwa sio mipango ya Mungu bali ya shetani.

"Magonjwa sio mpango wa Mungu bali ni hila za shetani ndio maana hata Ayubu alijaribiwa na shetani kupitia magonjwa na kwasababu sisi ni Binadamu kuugua ni ibada, inatukumbusha kwamba Mungu yupo na tunapaswa kumshukuru kwa kuendelea kutupa uhai kila iitwayo leo, hali unayoipitia niliwahi ipitia miaka miwili iliyopita lakini kwa sababu namuamini sana Mungu niliivuka, nakuombea sana @professorjaytz Mungu wetu ni waupendo na kwakua tunamwamini basi utapona," Aliandika Rose Muhando.