Nyota Ndogo afichua kwa nini ilimchukua mwaka 1 kukubali ombi la ndoa kutoka kwa mumewe

Muhtasari
  • Nyota Ndogo afichua kwa nini ilimchukua mwaka 1 kukubali ombi la ndoa kutoka kwa mumewe
nyota ndogo
nyota ndogo

 Mwanamuziki mashuhuri wa Kenya, Nyota Ndogo, amezua taharuki tena mtandaoni. Hii ni baada ya kufichua hadharani sababu kuu iliyomfanya achukue mwaka mmoja kukubali ombi la ndoa kutoka kwa mumewe Mzungu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nyota Ndogo alisema kutokana na neno kwenda tayari alikuwa akimpenda mume wake wa Uholanzi, Nielsen, lakini alipomuuliza endapo ataolewa naye alichukua muda wa mwaka mmoja kukubali ombi.

Nyota alisema sababu kubwa iliyomfanya afanye hivyo licha ya kumpenda sana ni kutotaka kuonekana amefanya uamuzi wa haraka kwa maana nyingine ni nafuu sana.

Kwa hiyo ilimbidi anunue muda na kufikiri vizuri sana, na haya yote yalimchukua mwaka mmoja kabla ya kusema ndiyo.

"This song imeshindwa kunitoka kichwani jamani kila nikiusikiza unanikumbusha the time mume wangu aliniuluza will you marry me Mwanaisha then nikachukua mwaka mzima kumjibu but nilikua nimekufa nimeoza unajua ukijibu haraka haraka ataona unaspeed nyingi.this song inanifanya nijiskie kumpenda mume wangu zaidi," Alisema Nyota Ndogo.