logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Churchill show yagura NTV yapata makao mapya TV47

Churchill show yagura NTV na kupata makao mapya katika runinga ya TV 47.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 March 2022 - 06:29

Muhtasari


  • • Baada ya kuzama kwa muda mrefu, hatimaye Churchill show imepata makao mapya ndani ya runinga ya TV47.
  • • "Imekuwa zaidi ya miaka kumi si ndio? Hiyo stori tutaitoa wakati MWENGINE," Churchill alisema.
Instagram, KWA HISANI

Baada ya kuzama kwa muda mrefu, hatimaye Churchill show imepata makao mapya ndani ya runinga ya TV47.

Hii ni baada ya kutamatisha mkataba wake na runinga ya NTV ambao umedumu kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo mashabiki wamekuwa wakipokea Burudani kutoka kwa wacheshi mbalimbali.

Kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, Churchill alisema kwamba imekuwa safari yenye changamoto, faida na mafunzo si haba huku akishukuru kila mmoja ambaye alitoa mchango kuhakikisha anaafikis ndoto yake ya kukuza vipaji na kuburudisha Wakenya.

"Imekuwa zaidi ya miaka kumi si ndio? Hiyo stori tutaitoa wakati MWENGINE," Churchill alisema.

Aidha, alisema kwamba anafurahi kwamba hatimaye wamepata makao mapya na kuwahakikishia mashabiki kwamba watazidi kupokea burudani Kali.

Pia alishukuru usimamizi wa TV47 kwa kumpa jukwaa na kuaminia kazi yake, huku akiahidi kuchapa kazi ili kuinua viwango vya stesheni hiyo hata zaidi.

Baadhi ya wacheshi Kama vile Sleepy David alionyesha furaha yake kwenye mitandao, huku aliwataka mashabiki kuwa tayari kwani wameandaa bonge la shoo, kuanzia tarehe 19 mwezi huu wa Machi.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wanahisi kwamba Churchill alichukua hatua mbaya ikilinganishwa kwamba NTV ilikuwa katika viwango vya juu zaidi kuliko TV47.

Kwa Sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona kipindi hicho kitafanya vipi pindi kitakapoanza kuruka hewani moja kwa moja.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved