'Kuzeeka ni asili,'Esther Musila kwa wanaokejeli umri wake

Muhtasari
  • Esther Musila ambaye ni mke wa Guardian Angel  kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewajibu moja kwa moja watu ambao wamekuwa wakimkejeli kwa ajili ya umri wake

Esther Musila ambaye ni mke wa Guardian Angel  kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewajibu moja kwa moja watu ambao wamekuwa wakimkejeli kwa ajili ya umri wake.

Esther Musila 52 anajulikana kuwa ameolewa na Angel 32. Esther Musila ni umri wa miaka 20 kuliko mume wake.

KUlingana na Esther kuzeeka ni asili na kwamba ila mtu atazeeka.

"Kuzeeka ni ya asili, na hiyo itatokea kwa sisi sote ... Ninataka tu kuangalia kama mimi mwenyewe, hata kama hiyo ni toleo la uzee,kwa hivyo furahia maisha yako wacheni nifurahie maisha yangu Kesho haijahakikishiwa yeyote kati yetu." Esther alisema.

Esther na Guardian walifunga pingu za maisha miezi chache iliyopita, huku harusi yao ikihudhuriwa na watu wachache na waliokuwa wamealikwa.

Esther Musila ana watoto watatu.