Muhubiri Ng'ang'a asema haya kuhusu video iliyooenea akimuombea msanii Rose Muhando

Muhtasari
  • Mchungaji Ng'ang'a hatimaye amezunumzia video inayomuonyesha akitoa pepo kutoka kwa msanii wa Tanzania, Rose Muhando
Mhubiri James Nganga akitoa hotuba katika harusi ya bintiye mnamo Machi 19, 2022
Image: WILFRED NYANGARESI

Mchungaji Ng'ang'a hatimaye amezunumzia video inayomuonyesha akitoa pepo kutoka kwa msanii wa Tanzania, Rose Muhando.

Video hiyo iliacha ndimi zikitetereka baada ya kugonga mitandao ya kijamii na yote kwa sababu zisizo sahihi.

Katika mahojiano ya kipekee na Mpasho, Ng'ang'a anasema watu waliiondoa video hiyo nje ya muktadha kwani ilihusisha mtu mashuhuri.

"Sina shida na Rose Muhando. Kuna wakati alinipigia simu na kunishukuru akisema amepona. Naombea watu mbalimbali.

Muhando ni nani? Yeye ni mtu kama mtu mwingine yeyote kwa nini anamlenga. Kwa nini usiulize kuhusu watu wanaougua saratani ambao nimewaombea?

Tunapoenda kwenye huduma kila mtu ni kondoo. Alivuma tu kwa sababu yeye ni msanii. Video ilivuma kimakosa," Alieleza Ng'ang'a

Muhubiri huyo aliendelea kutoa mfano wa mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka mingi na licha ya yote yesu alimponya hadharani, huku akisema kwamba hamna mtu mdogo wala mkubwa mbele ya Munu.

"Mbele za Mungu, hakuna mkubwa zaidi ya mwingine. Hata Yesu alimponya mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka mingi hadharani ikiwa kuna kamera wakati huo tungemuona. hakumuombea hadharani watu wangejuaje kuwa mtu wa aina ya Muhando anaweza kuugua na kupona?

Sasa anajulikana zaidi kuliko hapo awali."