Mamake Steven Kanumba amvulia kofia Diamond kwa kumsherehekea marehemu mwanawe

Muhtasari

•Mjane huyo amesema aliridhishwa sana na kitendo cha  Diamond kumsherehekea mwanawe hasa katika kipindi hiki cha kumbukumbu ya kifo chake.

•Katika wimbo wake 'Nawaza', Diamond alisema  "Huenda Kanumba angelikuwepo hai, Nawaza movie zetu pia tungejidai."

Diamond Platnumz na marehemu Steven Kanumba
Diamond Platnumz na marehemu Steven Kanumba
Image: HISANI

Bi Flora Mutegoa ametoa shukrani kubwa kwa bosi wa WCB, Diamond Platnumz kwa kumkumbuka marehemu mwanawe, Steven Kanumba katika wimbo wake wa hivi majuzi 'nawaza'.

Mjane huyo amesema aliridhishwa sana na kitendo cha  Diamond kumsherehekea mwanawe hasa katika kipindi hiki cha kumbukumbu ya kifo chake.

"Ameweza kumkumbuka marehemu Steven Charles Kanumba. Haikuwa rahisi. Nilipousikia nilifarijika, nilifurahi sana, kumbe bado anamkumbuka! Mwezi ujao, tarehe saba tunamaliza  miaka kumi," Bi Mutegoa alisema akihutubia waandishi wa habari.

Mutegoa alisema ni jambo la maana kuona Diamond anamuwaza marehemu mwanawe kwani ni wengi ambao tayari wamemsahau mwigizaji huyo ambaye alishabikiwa sana kote duniani.

Kanumba alifariki mnamo Aprili 7, 2012 kutokana na jeraha la kichwa baada ya kuanguka katika chumba chake cha kulala. Aliyekuwa mpenziwe, mwigizaji Elizabeth Michael alishtumiwa kwa mauaji yake na kushtakiwa kwa jaribio la mauaji.

Katika wimbo wake 'Nawaza', Diamond alisema  "Huenda Kanumba angelikuwepo hai, Nawaza movie zetu pia tungejidai."

Mamake Kanumba pia alitoa ombi kwa Diamond kumsaidia mwanawe mdogo, Seth Bosco, katika safari yake ya usanii