logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mna ujinga!" Cardi B awajibu mashabiki na kujiondoa Twitter, Instagram baada ya familia yake kutukanwa

Cardi B ajiondoa Twitter, Instagram baada ya mashabiki kumkejeli yeye na watoto wake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 April 2022 - 07:18

Muhtasari


  • • Kulingana na jarida la Billboard, mwanamama huyo alifikia uamuzi huu baada ya watukanaji wa mitandaoni kuvuka mipaka na kuelekeza michambo yao mpaka kwa familia yake.
Mwanamuziki Cardi B

Mwanamuziki wa Kimarekani Cardi B amechukua hatua ambayo haikutarajiwa na wengi baada ya kuzifunga kurasa zake katika mitandao ya Twitter na Insagram baada ya mashabiki wengi wa muziki kumjia juu kwa kukosa kuhudhuria hafla ya tuzo za Grammy zilizofanyika hivi majuzi.

Mwanamuziki huyo wa mitindo ya kufoka aliamua kuchukua likizo kutoka mitandao hiyo ambapo ndio ilifurisha jumbe za kumchamba na kumsimanga vikali baada ya kutohudhuria Grammy, hata kama awali hakuwa ameweka wazi iwapo angehudhuria.

Ilibidi amefanya jaribio la kujibu mipigo ya mashabiki hao ambapo alisema ni upuuzi kwa watu kumkejeli kwa kutohudhuria hafla hizo lakini ni kama vishindo vya mashabiki vilimkaba kwenye koo ikabidi amesalimu amri kwa kujiondoa mitandaoni humo.

Kulingana na jarida la Billboard, mwanamama huyo alifikia uamuzi huu baada ya watukanaji wa mitandaoni kuvuka mipaka na kuelekeza michambo yao mpaka kwa familia yake, jambo ambalo lilimuuma mno mpaka kupelekea kujitoa Twitter na Instagram.

Inasemekana rappa huyo alidinda kuhudhuria kwenye tuzo za Grammy kwa kile alisema kwamba hakuwa na albamu mpya ya kutambulisha, licha ya kuteuliwa kuwania kitengo cha Best Rap Performance.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved