"Ni chombo hatari!" Esma Platnumz amsifia mpenzi mpya wa kakake Diamond, afichua mipango ya ndoa

Muhtasari

•Esma alifichua kwamba familia yao iliweza kukutana na mchumba huyo mpya wa kakake Diamond Platnumz.

•Esma alifichua kwamba mipango ya ndoa inaendelea huku akieleza kuwa tayari barua ya kupeleka kwa wakwe wao ipo tayari.

Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Mfanyibiashara Esma Platnumz amefichua ni kweli kuwa hatimaye kaka yake Diamond Platnumz amejinyakulia kipenzi kipya.

Akiwa kwenye mazungumzo ya simu na mtangazaji Juma Lokole, Esma alifichua kwamba familia yao iliweza kukutana na mchumba huyo mpya wa kakake.

Mama huyo wa watoto wawili aliusifia sana urembo wa malkia huyo mpya kwenye familia yao huku akikiri kwamba iliwapata kwa mshangao.

"Ni chombo hataro! Jamani kuna watu wanakuwanga na bahati zao. Watu watahangaika kweli, hawatalala. Lakini kweli kila mtu Mungu kamwandikia. Sisi wenyewe hatujaamini lakini ametuhakikishia 100%," Esma alisema

Esma alifichua kwamba mipango ya ndoa inaendelea huku akieleza kuwa tayari barua ya kupeleka kwa wakwe wao ipo tayari.

"Barua tayari iko mezani. Mwenyewe atafunguka. Lakini ni chombo hatari," Alisema.

Ingawa hakufichua mengi zaidi kuhusu mchumba huyo mpya wa Diamond, Esma alidokeza kwamba familia yao imeridhika naye na ipo tayari kumkaribisha.