Simon Kabu akana kuwa na Sidechick, huku uvumi wa kuachana na mkewe ukienea

Muhtasari
  • Simon Kabu akana kuwa na Sidechick, huku uvumi wa kuachana na mkewe ukienea
Simon Kabu na mkewe Sarah Kabu
Simon Kabu na mkewe Sarah Kabu
Image: HISANI

Katika siku chache zilizopita, wamiliki wa Kampuni ya Bonfire Adventures Travel, ambao ni Sarah Kabu na Simon Kabu wamekuwa wakivuma baada ya machapisho  kudai kuwa hawakuwa na uhusiano mzuri.

Yote yalianza baada ya Sarah Kabu kuchapisha mitandaoni kuhusu ndoa yake yenye sumu akidai kuwa amekuwa akimficha mumewe sana lakini ilifika wakati afichuliwe.

Alisema kuwa Simon Kabu amekuwa akimkandamiza sana na hata alikimbia na watoto ambao walikuwa wamekabidhiwa kwa mwanamke mwingine ambaye hamfahamu.

Sarah Kabu alikuwa na huzuni na alisema kuwa kwa sasa hajui waliko watoto wake.

Chapisho hili lilivuma mitandaoni na watu walimweka wazi Simon Kabu kwa kumdanganya mkewe.

Siku ya Jumanne aliamua kutangamana na mashabiki wake mitandaoni na akawaruhusu kumuuliza maswali.

Alifichua wazi kuwa ana binti wa miaka 24 ambaye alimlea kabla ya kuoa na 

Simon Kabu aliendelea na kufichua kuwa hana 'side chick' na kwamba hamdanganyi mke wake na mtu yeyote kwa sababu anamheshimu.

Alimaliza kwa kusema kuwa ndoa yake iko sawa na wapo katika hali nzuri.