Mambo ya ajabu ambayo Harmonize amefanya kumtongoza Kajala amrudie

Muhtasari

• Harmonize alifichua hali ya kumpeza Kajala na ukweli kwamba bado anampenda kulichangia katika kuachana kwake na Briana.

•Kando na kununua zawadi za thamani, Harmonize pia amekuwa akimwomba msamaha hadharani mpenzi huyo wake wa zamani.

Harmonize na Kajala Masanja
Harmonize na Kajala Masanja
Image: HISANI

Siku za hivi majuzi mwanamuziki Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amekuwa akitia juhudi kubwa kumshawishi aliyekuwa mpenziwe Fridah Kajala Masanja warudiane.

Harmonize alianza kuashiria dalili za kumpeza Kajala takriban mwezi mmoja uliopita hata kabla ya kutangaza utengano wake na Briana Jai.

Hapo awali, Harmonize alifichua hali ya kumpeza Kajala na ukweli kwamba bado anampenda kulichangia katika kuachana kwake na Briana.

"Hatuko pamoja na Briana sababu moja nilimwambia nimetengana na mtu bila kugombana na nampenda sanaa sasa sina uhakika kama nimemove on, lolote linaweza kutokea,"Harmonize alisema.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Harmonize aliweka bango lake na mwigizaji huyo katika eneo la Kinondoni. 

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisema bango hilo lenye maandishi 'Lovers' lilimgharimu shilingi milioni 12  za Tanzania. (Ksh 600,000)

"Niliweka mimi 100%. Nilitumia milioni 12. Itakuwa pale kwa takriban miezi sita," Harmonize alisema.

Mapema mwezi Aprili, mwanamuziki huyo alienda katika duka la vito na kutambua mkufu wa thamani ambao Kajala aliokuwa ameupenda Kajala.  Harmonize alifichua alitumia shilingi milioni tano za Tanzania kupata cheni hiyo.

"Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu unayependa. Wakupeleka sasa? 5M kwa dhahabu," Alisema Harmonize.

Hivi majuzi Harmonize alinunua picha ya mpenzi huyo wake wa zamani na kuitundika katika chumba chake cha kulala.

Harmonize alisema alipiga hatua hiyo ili kila asubuhi anapoamka awe anakutana na sura ya mwigizaji huyo.

Wewe ndiye mtu pekee nitaona nikifungua macho yangu kila siku. Tafadhali rudi. Tabasamu kwa ajili yangu popote ulipo!!.. Nirudie tena" Harmonize alisema.

Siku ya Jumatano mwanamuziki huyo alitangaza kwamba amemnunulia Kajala Range Rover na kudai kuwa hilo ndilo gari la ndoto zake.

Konde Boy alisema alimtaka Kajala afahamu kuwa anayajuta sana maovu aliyomtendea pamoja na familia yake hadi kupelekea kuvunjika kwa mahusiano yao

"Inaeleza Majuto Ya Yote Niliyo Kufanyia !!!! Ninacho omba Kwako ni Msamaha wa thati Ya Moyo Wako !!!! Frida wewe ni Mtu Wa Mungu Sanaa!!! Unasali Pia Bila shaka Unatambua Hakuna Mkamilifu Hutokuja Kuanza Upya Mama. Unanifahamu zaidi, rudi tena. Usisahau Mimi ni Mtoto wa Masikini Mwenzio Tu.  Nina Familia ,Wajomba, Shangazi Wadogo Na Ndugu Kibao Masikini Ambao Nikifa Leo Ndio Watakao Nizika Ila Nimeona Wewe Ndo Unastahili," Harmonize alimwandikia Kajala.

Gari alilonunua Harmonize limesajiliwa kwa nambari KAJALA 1 GP kuashiria kwamba alinunua maalum kwa mwigizaji ambaye alichumbiana naye kwa miezi michache tu.

Kando na kununua zawadi za thamani, Harmonize pia amekuwa akimwomba msamaha hadharani mama huyo wa mpenzi wa Rayvanny, Paula Kajala.