'Alinifukuza kama mbwa,'Mcheshi Consumator azungumzia changamoto alizopitia

Muhtasari
  • Mcheshi Consumator azungumzia changamoto alizopitia
Consumator
Consumator
Image: Instagram, KWA HISANI

Mchekeshaji, Consumator amefunguka kuhusu jinsi alivyofukuzwa kama mbwa na rafiki yake.

Wakati huo mcheshi wa Churchill alisema alianza kuishi na rafiki yake baada ya Covid-19 kuja na hakuweza kumudu kulipa kodi peke yake.

Alikubali kugawana kodi na rafiki yake.

"Mwishoni mwa mwaka wa 2019, baba yangu alipatikana na saratani ya tezi dume. Lilikuwa jambo zito hivyo niliishia kutumia kiasi kikubwa cha akiba yangu, nashukuru sasa yuko sawa ingawa huenda kliniki mara kwa mara.

Baada ya hapo, sikuweza kumudu kulipa kodi kwa hivyo nikahamia kwa rafiki ambaye pia yuko kwenye tasnia hii. Tulikubali kugawana gharama ya kodi ya 3K. Wakati huo nilitarajia ningepata pesa lakini sikupata, lakini ndipo Covid-19 ilipotokea."

Mcheshi huyo aliweka wazi kwamba alifanikiwa kulipa kodi ya mwezi mmoja tu.

“Nilifanikiwa kulipa mwezi wa kwanza lakini sikuweza kulipa miezi michache iliyofuata (3) alianza kunionyesha madharau, akirudi nyumbani akiwa ameshiba na kulala, nilikuwa nalala njaa kwa sababu baadhi ya siku zingine sikuwa napata pesa hivyo basi kunilazimu kulala hivyo

Siku moja nilirudi nyumbani usiku nilikuta kila kitu kimetupwa nje ikiwa ni pamoja na nguo zangu za ndani. Sikuwahi kufikiria kwamba angeenda mbali kama tulivyokua pamoja."

Mcheshi huyo anasema kurushwa nje usiku na rafiki yake ilikuwa hatua ya chini kabisa maishani mwake.

“Nilidhani atanitupa nje kwa njia ya kidiplomasia, watu walikuwa wananifahamu hivyo ilikuwa ni aibu sana kuokota vitu huku watu wakitazama, siku hiyo nililala kwa mlinzi."

Pia mcheshi huyo aliweka wazi kwamba anapeza kuwa kwenye jukwaa, ili uwachekesha mashabiki wake.