'Wapende watu wangali hai,'Betty Kyallo asema huku akimuomboleza dada yake Waihiga Mwaura

Muhtasari
  • Kumpoteza mtu umpendayo ni moja wapo wa pigo kubwa kwa kila binadamu duniani, ilhali hawakukosea wliposema kuzaiwa bahati haya basi kufa ni lazima
Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Kumpoteza mtu umpendayo ni moja wapo wa pigo kubwa kwa kila binadamu duniani, ilhali hawakukosea wliposema kuzaiwa bahati haya basi kufa ni lazima.

Kila mmoja wetu atapitia katika njia hiyo, ilikuwa siku ndefu kwa wanandoa Joyce Omondi na Waihiga Mwaura siku ya JUmanne baada ya kumpoteza dada yake mdogo.

Huku mkewe Mwaura, Joyce Omondi akiomboleza kifo chake alisema kwamba matumaini yake yako kwa mola hasa wakati huu wanapitia kipindi kugumu.

"Katika Kristo pekee tumaini langu linapatikana Yeye ni nuru yangu, nguvu zangu, wimbo wangu Jiwe hili la msingi, ardhi hii thabiti Imara katika ukame na dhoruba kali zaidi Ni urefu gani wa upendo, ni kina gani cha amani Hofu inapotulia, mapambano yanapokoma Mfariji wangu, yote yangu katika yote Hapa katika upendo wa Kristo nasimama," Ulisoma ujumbe wake Joyce.

Mfanyibiashara Betty Kyallo akimuomboleza Gathoni alisema walikuwa marafiki wa karibu sana walipokuwa chuo kikuu.

"Haya yanauma Gath alikuwa mmoja wa wanadamu wazuri, tulikuwa marafiki wa karibu chuo kikuu, lala salama Gathy, ulikuwa wa baraka

Penda watu wangali hai, ishi maisha kikamilifu," Betty Aliandika.