'Kenya sio yetu,'Thee Pluto amwambia Bahati baada ya madai ya kujiuzulu

Muhtasari
  • Bahati alikuwa amepewa tikiti kutoka kwa chama cha jubilee kuwania ubunge wa eneo bunge la Mathare
Kevin Bahati
Image: WILFRED NYANGARESI

Msanii Bahati amezua hisia tofauti mitandaoni baada ya kulilia haki, baada ya kudai kwamba ameambiwa ajiuzulu kutoka kuwania kiti cha ubunge cha Mathare.

Bahati alikuwa amepewa tikiti kutoka kwa chama cha jubilee kuwania ubunge wa eneo bunge la Mathare.

Bahati alisema kuwa anawaheshimu Uhuru Kenyatta na Raila Odinga lakini wanapaswa kuwapa vijana nafasi.

Aliongeza kuwa Mathare imekuwa ngome ya ODM lakini kwa kuwa anawania kwa tikiti ya Jubilee anaomba nafasi.

Bahati aliongeza kuwa watu wa Mathare wapewe nafasi ya kuwa na kiongozi waliyemtaka siku zote.

"Ninakuheshimu Rais wangu na ninamheshimu Raila Odinga lakini tafadhali uwape vijana wa nchi hii nafasi. Najua Mathare imekuwa ikimilikiwa kama eneo la ODM lakini kwa hili wakati mmoja, wapeni vijana wa nchi hii nafasi. Wapeni watu wa Mathare kiongozi ambaye wamekuwa wakimtaka siku zote," Bahati alisema.

Huku muunda maudhui na mwana youtuber Thee Pluto akitoa hisia zake kuhusu jambo hilo alimwambia Bahati kwamba nchi ya kenya sio yake, na anapaswa kuazoe kwani ni jambo la kawaida nchini.

"Kenya si yetu tena, yaani unashinda fair na bado unambia ujiuzulu na wenye chama, kweli kenya ina wenye kusema," Aliandika Thee Pluto.