Sitaki kumvutia Delilah,'Willy Paul atoa sababu ya kunyoa dreadlocks zake

Muhtasari
  • Kwa mara ya kwanza, msanii huyo amejibu swali kwa nini alikata dreadlocks zake na hakusita kulikabili ana kwa ana na swali hilo
Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Wilson Abubakar Radido anayejulikana kama Willy Paul aliwashangaza wanamitandao alipokata dreadlocks zake na hakuacha sababu ya kuzikata.

Kwa mara ya kwanza, msanii huyo amejibu swali kwa nini alikata dreadlocks zake na hakusita kulikabili ana kwa ana na swali hilo.

Sababu moja kubwa aliyoitoa ni kutaka kuwa mtu aliyebadilika na kubaki kuwa mtu mzuri kama alivyokuwa au hata kuwa bora zaidi.

Alipoulizwa ikiwa dreadlocks zilimfanya awe mtu mbaya, Willy Paul aliamua kujibu swali hilo kwa kutoa kielezi kutoka katika hadithi maarufu ya Samsoni na Delila.

Alisema kuwa ni nywele zilizomvutia Delila kwa Samsoni na hataki kumvutia Delila yeyote ambaye atamshusha.

Kuhusu kwa nini alirudi kwenye sura yake ya zamani, Willy alisema kuwa anaipenda na haijaunganishwa nayo sana.

Hivi majuzi, Willy Paul amekuwa akifanya harakati za kimya kimya na amefichua kuwa anafanya kazi kubwa lakini ana mpango wa kushiriki na umma kuhusu hilo hivi karibuni.

"Niliondoa dhambi. Nilitaka kuwa mvulana mzuri, kijana wa mungu. Niliamua kuachana na kitu ambacho Delila angeweza kuona na kuja kukifanya.

Nimeona mengi, na nimepitia mengi mambo mengi yamechangia mimi kunyoa nywele zangu," Aliongea Willy Paul.