Wawachane na wake za watu,'Hisia za Ringtone baada ya mti kuangukia magari Naivasha

Muhtasari
  • Hisia za Ringtone baada ya mti kuangukia magari Naivasha
Image: Hisani

Familia kadhaa zinahesabu hasara inayofikia mamilioni ya pesa baada ya mti kuanguka kwenye magari yao wakati wa mapumziko ya wikendi huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru.

Kile ambacho kilidhaniwa kuwa wikendi ndefu kwa tafrija na uhusiano mwema kiligeuzwa kuwa vilio kwa familia hizo kufuatia kisa cha Camp Carnelley's kwenye ufuo wa Ziwa Naivasha.

Wakati wa tukio la Jumapili jioni, takriban magari matano yaliharibiwa na mtu mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya mti wa mshita kung'olewa na upepo mkali.

Mtu aliyejeruhiwa alikimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya lakini anaendelea vizuri huku wamiliki wa gari lililoathiriwa na wasimamizi wa hoteli wakiingia kutathmini uharibifu.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Naivasha Mutua Kisilu alithibitisha kuwa upepo mkali ulilazimisha mti wa mshita uliozeeka kuanguka na kuwalazimu makumi ya watu waliokuwa wamekita kambi katika hoteli hiyo kukimbilia usalama wao.

Huku msanii Ringtone akitoa hisia kuhusu tukio hilo alisema kwmba watu wnapaswa kutubu dhambi zao, na kuacha kujiviinjari na wake wa wenzio.

"PEOPLE THEY STEAL WIFES, GIRLFRIEND AND FIANCE OF PEOPLE AND GO EATING THEM AND GOD IS WHO HE IS WORKED IN MIRACLE WAYS. WATU WATUBU DHAMBI NA WAWACHANE NA WANAWAKE WA WENZIO HII NI ONYO YA MUNGU. πŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈ," Ringtone Aliandika