Inawezekana kupenda wanaume 3 kwa wakati mmoja kwa madhumuni tofauti-Huddah Monroe asema

Muhtasari
  • Aidha amewashambulia wanaume ambao wanadhani kuwa mwanamke hawezi kampenda mwanamume mwingine kwa sababu anampenda
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti maarufu nchini amekwa akivuma mitandaoni baada ya kuuza bidhaa za kuwasaidia wanawake, hasa wakati wanume wao wanasoma katiba.

Huddah anafahamika sana kutokana na matamshi yake mitandaoni, huku matamshi yake mengi akiwakejeli wanaume Wakenya kwa kusema kwamba hawajui mapenzi.

Mapema wiki hii mwanasosholaiti huyo alivuma mitandaoni baada ya kudai kwama anataka kuunganishwa na mwanariadha maarufu Omanyala.

Huku akizungumzia maoni hasi kuhusu bidhaa zake yaliyotolewa na baadhi ya Wakenya Huddah alidai kwamba Wakenya ni washamba, kwa kujifanya kujua kila kitu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Huddah amesema kwamba inawezekana kupenda wanaume 3 au wanawakekwa wakati mmoja lakini kwa madhumuni tofauti.

Aidha amewashambulia wanaume ambao wanadhani kuwa mwanamke hawezi kampenda mwanamume mwingine kwa sababu anampenda.

"Lol!Baadhi ya wanaume wanadhani kwa maana unawapenda huwezi penda mwanamume mwingine au umekata tamaa Inawezekana kupenda wanaume 3 au wanawake kwa wakati mmoja kwa madhumuni tofauti," Huddah Aliandika.