Wakenya waadhimisha siku ya kurudi kwa Stella

Muhtasari

•Wanamitandao nchini Kenya wametumia siku ya leo kuadhimisha jinsi Mwamburi alivyochengwa na mchumba wake Stella.

Kila mwaka inapofika siku kama hii, Mei 17, Wakenya huadhimisha siku ya  kurudi kwa Stella.

Stella ni msichana ambaye mwanamuziki mkongwe Freshley Mwamburi aliimbia katika kibao chake maarufu 'Stella Wangu.'

Katika kibao hicho alichotoa takriban miongo mitatu iliyopita, Mwamburi amesimulia masaibu yalikumba mahusiano yake baada ya mchumba wake kuenda ng'ambo kwa miaka mitatu.

Baada ya kuchumbiana kwa muda, mahusiano ya Mwamburi yalianza kutikisika baada ya Stella kuenda Japani kupata masomo ya Udaktari.

Mwamburi amesimulia jinsi alivyojitolea kwa hali na mali ili mradi tu Stella asafiri kuenda Japani lakini mwishowe mchumba huyo wake akamchenga.

"Nilikua na mchumba wangu

Tulipendana kama chama choma

Alibahatika kwenda ngambo

Chuo kikuu kwenda kusoma

Miaka mitatu kule Japani

Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilikua na mchumba wangu

Tulipendana kama chama choma

Alibahatika kwenda ngambo

Chuo kikuu kwenda kusoma

Miaka mitatu kule Japani

Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilivyo mpenda Stella jamani

Kajitolea kwa roho moja

Nikauza shamba langu

Sababu yake yeye

 

Nikauza gari langu, sababu yake yeye

Nikauza Ng'ombe na mbuzi sababu yake yeye

Ili apate nauli yake

Na pesa nyngine za matumizi kule Japani

Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano

Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano

Ndiyo ilokua tarehe kamili ya Stella kurudi Kenya

Nilikwenda uwanja wa ndege kwenda kumlaki Stella

Nilikua na uncle Kilinda uwnaja wa ndege

Nilikua baziri mwa Kolomba na mkewe na watoto wake

Nilikua uncle Mshomba wa mdundonyike tuveluva

Nilikua na ndugu Afisi mtoto wa Mombasa

Ghafla ndege lipotua uwanajani tuliona vituko

Stella alishuka amebeba mtoto mkononi

Nyuma yake mchumba wake mfupi

Futii nne Mjapani

Nilisikitika ndani ya moyo

Nikakosa la kufanya,"

Mwamburi ameendelea kusimulia jinsi alivyoangua kilio kikubwa baada ya kumuona Stella na familia yake mpya.

Licha ya yote bado anamsihi mwanadada huyo warudiane huku akimhakikishia kuwa bado anampenda.

Wanamitandao nchini Kenya wametumia siku ya leo kuadhimisha jinsi Mwamburi alivyochengwa na Stella wake.

Hizi baadhi ya jumbe: