Lilian Ng'ang'a awalaani waajiri wanaowalazimu vijakazi kuvalia sare za kazi nje ya nyumba

Muhtasari
  • Aliyekuwa mke wa gavana wa kaunti ya Machakos, Lilian Nganga wamekashifu waajiri wanaowalazimu viijkazi kuvaa sare zao za kazi nje ya nyumba
Image: INSTAGRAM// LILIAN NGANGA

Aliyekuwa mke wa gavana wa kaunti ya Machakos, Lilian Nganga wamekashifu waajiri wanaowalazimu viijkazi kuvaa sare zao za kazi nje ya nyumba.

Akiongea kupitia jukwaa lake la Instagram, Lilian alisema kuwa anawahukumu vikali watu wanaofanya wahudumu wa nyumba zao kuvaa sare kwenye mgahawa au maduka makubwa na sehemu nyingine za umma.

Lilian  alishiriki chapisho refu kwenye hadithi za Instagram ambapo alizungumzia jinsi inavyodhalilisha mtu kwenda mahali pa umma kama vile mkahawa au maduka makubwa akiwa amevaa sare.

"Inadhalilisha na kuona haifai mfanyikazi wako kuvalia sare zake za kazi kwenye maduka makubwa au kwenye umma, na wahukumu waaajiri sana sana vibaya," Alisema Lilian.

LIlian anonekana kuendele vyema na maisha yake baada ya kuachana na Mutua, huku kutengena kwao kukiibua hisia nyini mitandaoni.