Natafuta mganga wa kitambi-Boniface Mwangi

Muhtasari
  • Ni matamanio ya kila moja kuwa na mwili ambao unapeneza wakati wote, kwani tu,ewaona wengi wakikejeliwa mitandaoni kwa ajili ya miili yao
Mwanaharakati Boniface Mwangi
Image: Hisani

Ni matamanio ya kila moja kuwa na mwili ambao unapeneza wakati wote, kwani tu,ewaona wengi wakikejeliwa mitandaoni kwa ajili ya miili yao.

Wengi ambao wamepokea kejeli nyingi ni watu ambao wana miili nene, huku wengi wao wakikata tamaa na kuanza mazoezi kutokana na kejeli hizo.

Mwanaharakati Boniface Mwangi kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua kwamba anamtafuta mganga ambaye ataweza kupunguza kitambi chake.

Mwangi amekuwa akionekana akifanya mazoezi kila asubuhi ili  mwili wake uwe wa kupendeza.

Baba huyo wa watoto 3 anaonekana kukata tamaa kwani anazidi kukuwa na kitambi, huu hapa ujumbe wake uliowaacha wengi na kicheko.

"Natafuta mganga wa kitambi. Ule anatibu kitambi kutoraka haraka haraka. Dr. Make Stomach disappear wanted, client availablešŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£," Aliandika Boniface.