Anaongea-Profesa Jay aruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa siku 127

Muhtasari
  • Rapa huyo alilazwa mapema mwaka huu na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania
Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Image: HISANI

Baada ya siku 127 za kulazwa hospitali rappa maarufu kutoka Tanzania Profesa Jay hatimaye ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya hali yake ya afya kuimarika.

Kulingana na vyombo vya habari kutoka Tanzania Jay anaongea ilhali hana nguvu kwani muda huo wote amekuwa amelazwa.

Rapa huyo alilazwa mapema mwaka huu na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Jay alikuwa akifanyiwa dialysis kwani ini lake lilikuwa limeharibika. Pia alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Kulingana na Millard Ayo ambaye alitangaza habari izo njema kwa mashabiki wake alisema kuwa;

"Ni wengi walisikitika waliposikia hali ya afya ya Legend wa Bongofleva Joseph Haule Profesa Jay aliyelazwa Hospitalini kwa siku 127 haikuwa nzuri kiasi kwamba hata kuongea hakuwa anaweza, sasa baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali Familia yake imethibitisha kwamba Prof Jizze anaongea.

"Sasa hivi anaongea ila kwakuwa amekaa Hospitali sana hana nguvu kabisa anakuwa kachoka kwahiyo hata kumuongelesha hatupendi sana ili tusimchoshe"

"Amefurahi kupewa Tuzo, ile Tuzo ilimpa faraja kubwa sana nilipompelekea pale kitandani aliipokea akaikumbatia akaibusu hata Mimi nilimuona amefurahi sana pengine iliweza kumuongezea hata nguvu" ——— amesema Msemaji wa familia Black Rhino @blackchatta ambaye ni Mdogo wa Profesa J,"Ulisoma baadhi ya ujumbe wake.