Akothee akataa shinikizo la mitandao ya kijamii

Muhtasari

•Msanii huyo anajuta kuinunua Kifaa hicho kwa pesa mingi ilhali kwa sasa haoni umuhimu wake.

•Akothee anapenda maisha ya kifahari, na ana uwezo wa kufanya jambo lolote anachopenda.

•Kando na uwekezaji hapa nchini Kenya Akothee pia anadaiwa kumiliki Nyumba huko Uropa.

 

Image: HISANI

Akothee kupitia ukurasa wake wa Instagram ameapa kuwa hata sukumwa tena na Mtandao wa Kijamii kununua vitu zinazovuma Mtandaoni.

Mwanamuziki huyo amefichua kwamba hivi majuzi alinunua kifaa cha kuteleza kilichomgharibu Ksh45,000. Hii ni baada ya kifaa hicho kuzungumziwa sana mitandaoni.

"Kifaa hicho kwa sasa kimepoteza hadhi yake kwani kimekuwa cha kufanyia mazoezi nyumbani," Akothee alisema.

Msanii huyo amesema anajuta kukinunua kifaa hicho kwa pesa mingi ilhali kwa sasa haoni umuhimu wake.

'Ningejua ningetumia pesa hizi  kumlipia  Mwanafunzi yeyote Karo' Akothee alisema.

Akothee alidai kuwa watu wengi hukimbilia kununua vitu zinazovuma Mtandaoni alafu baada ya muda fulani  wanakosa kuona umuhimu wake na kuvitumia kwa kazi ambazo si zao.

Mwimbaji huyo mwenye mwaka wa 42 , ni mmoja  wa Wasanii tajiri zaidi katika eneo la Alfrika Mashariki.

Akothee anapenda maisha ya kifahari, na ana uwezo wa kufanya jambo lolote analopenda.

Mbali na Kazi yake ya muziki, Akothee pia mjasiriamali ambaye ana msururu wa kampuni ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Usafiri (Akothee Safaris), Akothee Foundation miongoni mwa zingine.

Pia anajivunia kuwa na nyumba mbalimbali,ikiwa ni pamoja na moja iliyoko Rongo,Kaunti ya Migori na nyingine huko Mombasa,ambako amara nyingi hukaa akiwa nchini.

Kando na uwekezaji hapa nchini Kenya Akothee pia anadaiwa kumiliki Nyumba huko Ulaya.

Nyumba hiyo ya vyumba vinne inadhaniwa kuwa iko karibu na mji mkuu wa Uswizi wa Zurich na pia imefafanuliwa kama Jumba la Akothee huko Uropa.