Ugonjwa wa baba yangu unanitia wasiwasi -Akothee

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano ameeleza kuwa baba yake amekuwa akishindwa kuhudhuria shoo zake.

•Mwanamuziki huyo alisema kuwa kudhoofka kwa afya ya babake ni jambo ambalo ameshindwa kuishi nalo

Mwanamuziki Akothee
Mwanamuziki Akothee
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamziki maarufu nchini Akothee ​​ amefunguka kuhusu ugonjwa wa baba yake ambao umekuwa ukimsononesha kila wakati.

Mama huyo wa watoto watano ameeleza kuwa baba yake amekuwa akishindwa kuhudhuria shoo zake.

''Mshauri wangu siwezi kuanza kuandika chochote, ninachojua ni kwamba wewe huji tena kwenye hafla zangu'' Akothee alisema wakati akimsherehekea mzazi huyo wake mnamo Father's Day.

'Nimelia sana, na bado sikatii tamaa'' aliongeza.

Akothee alisema wakati mwingine huwa anakosa ujasiri wa kuzungumza na babake kwa sababu ya hali yake, jambo ambalo anajaribu sana kukumbana nalo.

''Sizungumzi na wewe mara nyingi kama hapo awali kwa sababu nimeachwa nikijiuliza maswali mengi,'' Akothee alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa kudhoofka kwa afya ya babake ni jambo ambalo ameshindwa kuishi nalo, na hayuko  tayari kukubali hatima hii.

''Siamini jinsi ulivyo sasa hivi, haya si maisha ambayo ulikua umezoea kuishi '' Akothee alisema.

Mwanabiashara huyo pia alifichua  kuwa mawasiliano kati yake na babake kupitia simu yamekuwa finyu.

''Hatuongei kwa njia ya simu kama tulivyokuwa tunazungumza baba, sikutumi pesa, kwa sababu ukishakuwa na pesa unasahau mahali unapoweka pesa yako''Akothe alisema.

Akothee alidai kuwa hajui  ikiwa anapaswa kuendelea kuhifadhi  nambari ya simu ya babake  kwenye simu  yake ya mkono au kuifuta.

''Ninapaswa kufuta nambari  yako kutoka kwa  simu yangu  ama?'' Akothee alihoji.

''Mungu akuponye baba nakupenda na naninakukosa sana moyoni'' Alimalizia.

Mnamo Julai 4, Akothee alikaribisha familia na marafiki katika hafla ya kufana ya kuzindua kitabu chake 'Akothee Quotes.'

Waliopata nafasi ya kuhudhuria hafla hiyo ni pamoja na mamake mzazi, watoto wake, jamaa na marafiki zake. Baba yake hata hivyo hakuweza kuungana nao kwa sababu  ya hali yake mbaya ya kiafya.

Mwimbaji huyo amejiunga na orodha ya watu mashuhuri wa Kenya ambao wameandika vitabu miongoni mwao Janet Mbugua, Lupita Nyong’o, Polycarp Otieno wa Sauti Sol na Adele Onyango.