Akothee asema ametengana kimawazo na kihisia na Nelly Oaks

Muhtasari

•Kulingana na mwimbaji huyo, mahusiano hayakuwa yakimlemea tu bali pia yalimvuruga kiakili.

•Mama huyo wa watoto watano alieleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akitangaza kuachana na Nelly Oaks 

Akothee na mpenzi wake Nelly Oaks
Akothee na mpenzi wake Nelly Oaks
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamziki Akothee amefichua kuwa aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks kufuatia masuala yaliyokuwa yakiathiri afya yake.

Kulingana na mwimbaji huyo, mahusiano hayakuwa yakimlemea tu bali pia yalimvuruga kiakili.

Mama huyo wa watoto watano alieleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akitangaza kuachana na Nelly Oaks, akisema;

''Nimetoka kwenye mahusiano mengine yenye misukosuko tofauti, kwa hivyo hii ya mwisho isiwe ya kushangaza. Ni uamuzi wa kibinafsi tu, ninahitaji wakati wa  kufurahia maisha yangu mapya, ninahitaji kujishughulisha na kazi yangu, siko tayari kwa mahusiano yoyote, maswali, au majibu kwa kile kilichotokea.Sikutaka kuumiza mtu yoyote. lakini samahani ndivyo ilivyo''

Licha ya chapisho hilo la kuachana, madam boss aliweka wazi kuwa bado anamheshimu jamaa huyo kwani wana historia ndefu pamoja;

''Mimi na Bw. N tuna Uhusiano wa kifamilia huko Rongo. Kwa hilo tuiheshimu familia na tuitunze HESHIMA ya familia, Yeye sio mtu niliyemchagua tu mitaani. Kwa hivyo kwa jambo hilo nawatakia nyinyi nyote maisha bora''

Hata hivyo katika mahojiano ya hivi majuzi Akothee alisema alijitenga na Nelly Oaks mnamo Desemba 2021. Kwa hivyo kimsingi mwanamume huyo alikuwa kwenye uhusiano peke yake kwa miezi 6 bila kujua Akothee alishajitenga na yeye kimapenzi.

''Sitawahi kutangaza kuachana ikiwa mimi mwenyewe sijaamua . Hata watu mashuhuri wakubwa zaidi  wanapambana na uhusiano… kwa kweli, kulingana na mimi nilikuwa nimetoka kwenye uhusiano mnamo Desemba'' Akothee alisema.

Na nadhani hii inaelezea kwa nini wawili hao hawafuatiliani tena kwenye mitandao ya kijamii na kwa nini wamefuta picha za kila mmoja kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii pia.