Rasmi Lukamba msanii wa bongo fleva atengana na WCB

Muhtasari

•Rasmi Lukambi ambaye sasa ameachilia ngomba mpya 'Utacheka'

•Msani huyo lisema kuwa kuna wengi ambao wanatamani kufanya kolabo na yeye

Msanii wa Bongo fleva Rasmi Lukamba
Msanii wa Bongo fleva Rasmi Lukamba
Image: YOUTUBE

Msani wa Bongo fleva Rasmi Lukamba amehama kutoka WCB, mwanamuziki huyo aliwekahaya wazi wakati alikuwa akihojiwa na runinga ya Bongo5.

Rasmi Lukambi ambaye sasa ameachilia ngomba mpya 'Utacheka' umeanza kufanya mzuri sana.

''Mimi nimetoka shule, Wasafi ni shule ya muziki , ni mtindo gani ya kimuziki yenye sijui''Rasmi aliuliza.

Wakati huo huo, pia aliweka wazi kuwa wanamuziki kutoka afrika mashariki wasipokuwa waangalifu, muziki ya wasanii kutoka Nigeria itashindana nao kwa ukubwa sana.

''Wasanii wakitoa matabaka,itasaidia sana, Diamond ni msanii tajika, Alikiba vile vile,kila mtu ni mkubwa kwa njia moja au ingine,tusapotiane, nataka iwe kwamba Dioamond akipost ngoma za Alikiba leo, Alikiba pia kufanya vile vile'' Lukamba alisema

Msani huyo lisema kuwa kuna wengi ambao wanatamani kufanya kolabo na yeye, na kutoka kwake WCB, si kwa sababu ya chuki kati yake na Diamond.

''Niko ha haki ya kushabikia mwanamuziki yeyote, haimanishi kuwa nikishabikia Diamond sasa nachukia Alikiba'' Lukamba alisema.

Yeye ni mmoja kati ya vijana waliofanya kazi ya kupiga picha video (video grapher)  kuthaminiwa na kupewa heshima kubwa zaidi.

Lukamba alikuwa  ni mpiga picha na video wa  Diamond  lakini kabla ya hapo alikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji.

Tayari alishaanza kujishughulisha na masuala ya uigizaji ambapo Muandaaji wa filamu nchini, William Mtitu,alishamuandaa kumtoa katika filamu ambayo angecheza kama Hemed Phd wa pili.

Ndoto ya kuwa muigizaji mkubwa ilififia kutokana na maslahi, kumbe wakati huo Mungu alikuwa ameshafungua milango ya baraka.

Akiwa Katika Harakati za kutafuta nafasi ya kupenya WCB ,Lavalava alimfuata Lukamba ambaye alikuwa akiishi naye maeneo ya Bunju na kumuomba amshuti Kava ya wimbo wa Diamond ‘Utanipenda’.