Rudeboy na Mr. P wako tayari kutumbuiza mashabiki wao nchini Kenya

Muhtasari

•Peter na Paul walikuwa na nguvu kubwa katika tasnia ya muziki ya Nigeria kabla ya kutengana mnamo 2017.

•Hatimaye  madungu hao walisameheana tarehe 17 Novemba 2021.

Peter Okoye, Paul Okoye
Image: P-Square (Instagram)

Wanamuziki wawili mashuhuri Peter na Paul Okoye, wanaofahamika kwa jina lao la awali Psquare, wametangaza mipango ya kutumbuiza nchini Kenya.

Katika video ya instagram kwa akaonti ya Rudeboy, waimbaji ya kibao cha 'Do Me' walitangaza kuwa wanaanza ziara katika miji 100 duniani kote, Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, na London kati ya nchi nyingine.

''Unajua nini,ni wakati wa  Psquare na tutazuru miji 100 duniani kote,Kenya, Tanzania Afrika Mashariki kote, London, United States. Zitaje,nyimbo mbili mpya zinakuja '' Psquare walisema.

Psquare, ambao sasa wanajitambulisha kuwa Rudeboy na Bw. P baada ya kutengana kwa muda mfupi.

Watakuwa kwenye ziara yao ya kwanza nchini Kenya tangu maridhiano yao mwishoni mwa mwaka jana.

Ndugu hawa Peter na Paul walikuwa na nguvu kubwa katika tasnia ya muziki ya Nigeria kabla ya kutengana mnamo 2017.

Peter aliamua kuitwa Mr. P huku Paul akijitambulisha kwa jina la Rudeboy huku wakitumbuiza mashabiki wao  kwa kiwango cha juu sana wakati huo wa utengano.

Hatimaye  madungu hao walisameheana tarehe 17 Novemba 2021,na kumbatiana hadharani  huko Lagos.

Mke wa Peter na kaka mkubwa wa wawili hao, Jude Okoye  walikuwepo na kukumbatiana pia.

Mnamo 2001, "P-Square" ilishinda shindano la "Grab Da Mic", kutokana na hayo Benson na Hedges walifadhili albamu yao ya kwanza, iliyoitwa Last Nite.

 P-Square pia waliteuliwa kama "Most Promising African Group" katika Tuzo za Kora miezi mitatu baada ya kutolewa kwa albamu yao ya kwanza. Hatimaye walishinda Tuzo la Amen la 2003 la "Kikundi Bora cha R&B".