Ikitokea nimekufa bendera ya Tanzania haipo-Diamond ajisifia kuwa mwanamuziki bora Tanzania

Muhtasari
  • Huwa anajitaja kuwa bora zaidi nchini Tanzania, Afrika Mashariki na hata Afrika nzima
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa bongo Diamond Platnumz ni mwanamuziki wa Tanzania na muziki wake umeenea sehemu mbali mbali ulimwenguni.

Huwa anajitaja kuwa bora zaidi nchini Tanzania, Afrika Mashariki na hata Afrika nzima.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amerudia hilo ambapo alichapisha orodha iliyoandaliwa na Innocent Mjagi Kwenye Twitter ya wasanii kumi wa Afrika ambao Wana ushawishi mkubwa ulimwenguni.

Orodha hiyo imejaa wasanii wa Nigeria ambao wamechukua nafasi 8 na nyingine mbili zilizosalia ni za Diamond Platnumz na Fally Ipupa wa Congo.

Nambari mbili ni Davido, tatu Ckay, nne Diamond Platnumz na tano Kizz Daniel. Olamide, Fireboy, Rema, Fally Ipupa na Tems wanakamilisha orodha hiyo.

Baada ya kupakia orodha hiyo, mwanamuziki huyo amedai iwapo ataaga dunia leo, bendera ya Tanzania ya burudani haitakuwepo kwenye orodha hiyo.

“Kiufupu ikitokea nimekufa bendera ya Tanzania haipo hapo pengine top 100 Inshallah,"Aliandika Diamond.