Usikubali mtu yeyote akukejeli kwenye mtandao wako wa kijamii-Akothee kwa watu mashuhuri

Je umewahi kejeliwa mitandaoni na ulihisi vipi

Muhtasari
  • Aidha aliwashauri wanapaswa kuwapa watu kama hao block baada ya kukejeliwwa
Akothee

Tumewaona sio mmoja au wawili bali baadhi ya wasanii,waigiaji,waunda maudhui na watu mashuhuri wakilalamika na kusimulia jinsi wamekuwa wwakikejeliwa mitandaoni.

Kuna wale wanakejeliwa kwa mambo wanayoyafanya au kwa ajili ya kazi zao.

Msanii na mjasirimali maarufu nchini Esther Akoth almaarufufu Akothee kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri watu mashuhuri kuhusiana na kejeli za wanamitandao.

Kulingana na msanii huyo, wasanii na watu mashuhuri hawapaswi kukubali mtu yeyote kumkejeli kwenye ukurasa wake wa kijamii.

Aidha aliwashauri wanapaswa kuwapa watu kama hao block baada ya kukejeliwwa.

"Kwa mtu yeyote mashuhuri,usikubali mttu akukejeli kwenye ukurasa wako wa kijamii kwa saabu ya kile unapakia mtandaoni kuhusu maisha yako 

Wape block na akaunti nyingine ambayo watafungua," Aliandika Akothee.

Je umewahi kejeliwa mitandaoni na ulihisi vipi, kwani wengi huisia kupatwa na msongo wa mawazo.