Baada ya muigizaji Carrol Muthoni almaarufu Sonie kufichua kwamba baada ya kuachana na mchekeshaji Mulamwah sasa ako katika mahusiano mapya, muigizaji huyo sasa amekataa kabisa kwamba hatoweza kumutambulisha mchumba huyo wake mpya kwa jamii ya mitandaoni.
Akifanya hadhara ya kuliizwa na kujibu maswali kwenye Instagram yake, Carrol Sonie aliulizwa iwapo yupo tayari kumtambulisha mwanaume wake kwa mashabiki wake, jambo ambalo alilikemea mno na kusema kwa kile alichojifunza katika mahusiano yaliyofeli na Mulamwah, hawezi kutaka hata siku moja mwanaume wake kujulikana mitandaoni wala mahusiano yake kuwa wazi kama ambavyo walikuwa na Mulamwah.
“Utamtambulisha mchumba wako mpya lini kwetu sisi wanamitandao, hatuwezi ngoja kabisa,” mmoja alimuuliza.
“Heh Hapana, hii Nairobi ficha mtu wako kama bangi,” Sonie alijibu.
Katika mahusiano yake ya awali na mchekeshaji Mulamwah, muigizaji huyo alikuwa anajivinjari na mpenzi wake mitandaoni na kuelezea wanamitandao kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika mahusiano yake.
Pale ambapo walikuja kuvurugana, wawili hao walikandiana vibaya mno kwenye mitandao huku kila mmoja akitunga hadithi na maneno ya kumchafua mwenzake ili kujionesha kuwa mzuri aliyekosea.
Hatua ya Sonie kukataa kabisa kuonesha mwanaume wake mpya kwenye mitandao ya kijamii ni wazi kwamba alijifunza funzo la kudumu kutoka mahusiano yake ya awali, kwani kile alichopitia baada ya wanamitandao kujua kwamab wameachana kilikuwa cha kuvuruga akili vibaya sana.
Sonie na Mulamwah walibarikiwa na mtoto mmoja wa kike, mtoto ambaye pia walimtambulisha wazi mitandaoni na hilo baadae walipoachana lilizua mjadala mkali kwamab huenda mwanadada huyo alichepuka na baada ya Mulamwah kufshamu kwamba mtoto si wake ndio maana walitengana.
Kwa upande wake Mulamwah alisema kwamba Sonie alikuwa mtu wa kufukuzia na kutamani maisha ghali hali ya kuwa yeye alikuwa ni mtu wa kubana mahitaji ili kufanya miradi ya baadae kijijini mwao na kusema hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya kila mtu kujishughulisha na hamsini zake.
Sonie alimtaka Mulamwah kubakisha maneno ya akina na asiongee akamaliza kwani kuna leo na kesho na pindi wanapoendelea kuingiza mtoto katika vita vyao vya maneno basi kesho mtoto atakapokua atampa Sonie wakati mgumu kulazimika kujibu maswali mengine yasiyo ya maana kutokana na mdomo wa aliyekuwa mchumba wake Mulamwah.