Mwanasosholaiti Amber Ray anafahamika sana kwa ajili ya maisha yake ya mapenzi, kwani ameekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti wenye umaarufu mkubwa.
Kupitia wenye ukurasa wake wa instagram hasa kwenye Insta stories aliweka wazi kwamba hampendi mwanasosholaiti mwenzake Vera Sidika.
Amberay aliendelea kusema yeye hapendi mtazamo wa Vera. Wawili wao hawaonani jicho kwa jicho.
Inasemekana kwamba Amberay na Brown Mauzo walikuwa wapenzi wakati wa nyuma.
Shabiki mmoja alimuuliza mbona asisuluhishe ugomvi wake na aliyekuwa mke mwenza wake Amira, huu akisema kwamba hana tatizo na Amira
Aidha Amber amesema kwamba Amira alikuwa anamwekelea mambo, lakini kwa sasa anajua amejifunza.
"Sina shida naye, alikuwa ananiekelea kila kitu akijua vizuri kwamba sio mimi nilikuwa na shida,natumai anajua vizuri sasa,"Alijibu Amber.
Huku akijibu sababu ya kutozungumza na Vera alisema kuwa;
"Simpendi i find her fake na roho mbaya."