Wakenya watoa maoni kuhusu tangazo la Raila la Ugali wa buluu

Raila alipakia video ya matangazo kwa lengo la kuupigia debe muungano huo.

Muhtasari

•Ugali wa manjano ulionyeshwa ukiwa mdogo na watu wengi walisubiri kuula ilhali ule wa bluu ulikuwa mkubwa na wa kuwatosha watu wote.

•Kufikia wakati wa kuchapisha ripoti hii zaidi ya watumiaji 800 wa twitter walikuwa wametoa maoni yao. 

Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Alhamisi mgombea urais wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga alipakia video ya matangazo kwa lengo la kuupigia debe muungano huo.

Katika video hiyo iliyopakiwa kwenye akaunti yake ya Twitter na kunukuliwa 'Ugali ya Azimio itatosha Wakenya wote!', mchekeshaji Mdomo Baggy ambaye ndiye mhusika alilinganisha ugali mbili, wa rangi ya manjano na ugali wa bluu.

Ugali wa manjano ulionyeshwa ukiwa mdogo na watu wengi walisubiri kuula ilhali ule wa bluu ulikuwa mkubwa na wa kuwatosha watu wote.

"Mazee gharama ya maisha imepanda. Bei ya unga imekuwa ni noma mpaka ikifika ni saa ya kukula ni pressure!" Mdomo Baggy alisema katika video hiyo.

Aliukosoa ugali mdogo wa manjano na kuusifia ugali mkubwa wa bluu akisema unatosha familia nzima na hadi majirani.

"Tunaweza kuwa na ugali wa kutosha tukiwa na bei ya unga ambayo ni poa. Bibi yako akikula unamwambia ongeza. Mtoto akikula unamwambia ongeza. Jirani asipokuja unamwita akuje.. juu ugali itakuwa ya kutosha," Alisema.

Wakenya watumizi wa Twitter walijumuika chini ya tangazo hilo kutoa maoni yao huku wengi wakionekana kulikejeli.

Kufikia wakati wa kuchapisha ripoti hii zaidi ya watumiaji 800 wa twitter walikuwa wametoa maoni yao. 

Baadhi ya wanamitandao walikuwa na haya ya kusema;-

@YohanDok Lakini baba uko supreme Court leo wanatumaliza, ata ni heri umeleta hii story ya ugali vile wao wameenda lunch tukule kwa macho,juu weuuh!!!

@mbinya_1 Ugali ya Azimio na mliweka subsidy only four weeks enye ata haikufikia kila mtu?

@Yungeo_ Tweet hii inahusu ishara, sio kila kitu ni kuhusu chakula.