Rapa Cardi B ahukumiwa baada ya kukiri mashtaka ya shambulizi katika klabu ya utupu

Mwimbaji huyo allihukumiwa kifungo cha siku 15 katika huduma ya jamii.

Rapa huyo alikubali makubaliano ya kukiri siku moja kabla ya kesi yake kusikizwa
Rapa huyo alikubali makubaliano ya kukiri siku moja kabla ya kesi yake kusikizwa
Image: BBC

Cardi B amekiri makosa mawili yaliyotokana na ugomvi katika klabu ya utupu, kama sehemu ya makubaliano ambayo yanamaanisha kuwa ataepuka kesi na kufungwa jela.

Rapa huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy, mzaliwa wa Belcalis Almanzar, alikiri kosa la shambulio la kiwango cha tatu na kusababisha hatari kiwango cha daraja la pili, na alihukumiwa kifungo cha siku 15 katika huduma ya jamii.

Mashtaka mengine kumi yalitupiliwa mbali.

‘’Nimefanya maamuzi mabaya katika siku zangu zilizopita ambayo siogopi kukabiliana nayo na kuyasimamia,’’ alisema katika taarifa.

Mahakamani, kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 alikiri kuandaa na kushiriki katika mashambulizi mawili dhidi ya wafanyakazi wa klabu ya usiku ya Angels huko New York mnamo 2018.

Kulingana na mamlaka, matukio hayo yalikua ya ugomvi kati ya Almanzar na dada wawili - mmoja wao aliamini alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe, rapa Offset.