logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi sikuwa feki, Nafurahia jinsi mambo yanavyoendelea - Otile amkejeli Vera Sidika

Ilmradi mimi ninajua kuwa nilidumisha kuwa mkweli na asilia bila kuwa bandia, niko vizuri na jinsi mambo yanavyotokea - Otile Brown.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 October 2022 - 09:46

Muhtasari


  • • Sidika alimbwaga Otile Brown kwa kile wadaku walisema ni kutoridhika na jinsi Brown alikuwa anamdekeza katika sinia la mapenzi.
Otile Brown amchokoza Sidika

Msanii namba moja kwa miziki ya kizazi kipya nchini Kenya, Otile Brown amekuwa mtu maarufu wa hivi punde kurusha dongo kwa mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika baada ya kupakia picha mpya akiwa amepunguza makalio.

Jumatano, Vera Sidika aliweka wazi kupitia picha pamoja pia na maelezo marefu kuwa aliamua kuchukua uamuzi huo mgumu wa kupunguza shepu yake ya maungo kutokana na sababu za kiafya.

Sidika alisema kuwa upasuaji aliofanyiwa kuongeza makalio ulikuwa umeanza kumtafuta mpaka kulazimisha kufanyiwa upasuaji mwingine wa kupunguza makali mpaka shepu hiyo mpya aliyoonekana nayo na ambayo sasa imemgeuza kichekesho katika mitandao ya kijamii.

Wengi wanaofuatilia Sanaa ya Kenya wanajua kuwa miaka kadhaa nyuma msanii Otile Brown walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Vera Sidika, mahusiano ambayo hayakudumu kwa muda mrefu.

Sidika alimbwaga Otile Brown kwa kile wadaku walisema ni kutoridhika na jinsi Brown alikuwa anamdekeza katika sinia la mapenzi.

Otile Brown sasa ameibuka na ujumbe fiche kupitia instastory yake ambao unaonekana kumlenga moja kwa moja Vera Sidika kuhusu umbo lake la awali ambalo sasa imebainika lilikuwa la bandia.

“Ilmradi mimi ninajua kuwa nilidumisha kuwa mkweli na asilia bila kuwa bandia kwa njia yoyote kutoka upande wangu, niko vizuri na jinsi mambo yanavyozidi kuchanua,” Otile Brown alirusha bomu la moto kwenye makalio ya Sidika.

Sidika alikuwa mwanadada mwenye umbo la kutamanisha kila mwanaume ambaye alikuwa anampita, lazima angegeuka mara mbili mbili nyuma kusifia ‘kazi ya Mungu’ katika mwili wa Sidika – pasi na kujua kuwa ilikuwa bidii ya upasuaji baada ya upasuaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved