Aliyekuwa gavana wa Nairobi ,Mike Mbuvi Sonko ametoa maoni yake katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu muonekano mpya wa mwanasosholaiti Vera Sidika.
Sonko ameonekana kumhurumia Sidika kwa kupitia upasuaji wa kuyatoa makalio bandia aliyokuwa nayo ili aweze kubaki na makalio asili.
"Huyu Vera Sidika maskini karibu akufe," Sonko alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo, Sonko aliwapa wanawake tahadhari ya kutopenda miili yao na baadaye kuamua kufanyiwa upasuaji ili waonekane warembo zaidi.
Mfanyibiashara huyo alimtumia Sidika kama somo kwa wanawake baada ya mrembo huyo kutangaza kuwa makalio bandia aliyokuwa nayo yalimpa shida za kiafya na kumlazimu kuyaondoa kupitia upasuaji.
Aliwaambia wanawake waridhike na maumbile waliyopewa na Mungu ili kuzuia majuto huko mbeleni.
"Wacheni kufanya ukarabati wa makalio yenu,"Sonko alisema.
Bintiye Sonko, Sandra Mbuvi pia alikuwa ametoa maoni yake kuhusu upasuaji wa Sidika.
Aliwakosoa wanamitandao kwa kumkejeli mama huyo wa mtoto mmoja baada ya kupoteza kivutio chake cha watalii na hata mashabiki wake.
Sonko alisema kuwa hakufurahishwa na wanamitandao kwa kumhukumu Sidika, wakati alikuwa na makalio bandia na hata sasa baada ya kuyaondoa.
"Mbona mnachukulia kila jambo vibaya na kuona baya katika kila kitu? Inaudhi sana. Mlikuwa mnamhukumu Sidika alipokuwa na makalio makubwa kwa kuwa hakuwa na makalio asili na kuwa alikuwa amefanyiwa upasuaji ili kuyaongeza ila sasa ambapo ameamua kuwa na makalio asili na kufanyiwa upasuaji ili kutoa yale bandia mnamkejeli na kumshambulia kwa maneno mitandaoni," alisema.
Aliwaambia wanamitandao kuwa hata wasiporidhishwa na jambo lolote analofanya Sidika yeye hajamkosea mtu yeyote na kuwa ataweza kufaulu katika mikakati yake ya kila siku.