logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwakani nakuoa kabisa kwa harusi - Whozu amhakikishia Sepetu

Wapenzi hawa wawili wameonyesha kuwa kwenye mapenzi na kupendana kwa dhati

image
na Davis Ojiambo

Burudani12 October 2022 - 05:56

Muhtasari


  • • Alitumia pete na shela ya bibi harusi na mwaka wa 2023 kuashiria kutaka kufunga pingu za maisha na mwigizaji huyo.
  • • Mpenzi huyo wa Whozu alisema kuwa Whozu ndiye furaha yake na anayemfanya atabasamu huku akiweka ishara ya moyo.

Mwanamuziki Whozu ameashiria kufunga pingu za maisha na mwigizaji Wema Sepetu mwaka unaokuja wa 2023.

Whozu alidokeza maendeleo hayo kwa chapisho la Instagram kwenye ukurasa wa Sepetu na kumwita mke wake.

Alitumia pete na shela ya bibi harusi na mwaka wa 2023 kuashiria kutaka kufunga pingu za maisha na mwigizaji huyo.

"2023...mke wangu," Whozu alisema kwenye chapisho hilo.

Sepetu alikuwa amechapisha picha moja iliyoonyesha amekumbatiwa na mpenzi wake na kupigwa busu.

Aliwaambia mashabiki wake furaha aliyokuwa nayo kuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki huyo na kuwatakia usiku mwanana.

Mpenzi huyo wa Whozu alisema kuwa Whozu ndiye furaha yake na anayemfanya atabasamu huku akiweka ishara ya moyo nyekundu.

Mashabiki wake wengine walimwonyesha mwigizaji huyo upendo na kuwa wanafurahia maendeleo yake na Whozu huku wengine wakimkemea.

Sepetu alimsuta shabiki aliyejaribu kumkatisha tamaa na kutoa maoni hasi kuhusu uhusiano wake na Whozu.

"Litakukuta jambo uje utulilie hapa," shabiki huyo (dorriemushi) alisema akiashiria kumcheka Sepetu.

Mwigizaji huyo hakufurahishwa na maoni ya shabiki huyo na kumwambia kuwa hayo ni mipango ya Mungu na yeye tu ndiye anayejua kitakachofanyika.

"Wacha kuombea watu mabaya, kikubwa ni furaha yangu," Sepetu alimfokea shabiki huyo ambaye alionekana kutofurahia mapenzi wa wawili hao.

Mashabiki wengine waliendelea kuibua gumzo baina yao na kumuunga mkono Dorrie na kusema kuwa Sepetu atakuwa na majuto baadaye.

"Furaha bila mtoto, tulia bibi. Wewe utapigwa tukio na huyo kijana na hilo tukio tusipokuzika basi tena, unatakiwa kujua upo na Whozu kwa muda tu kwahiyo furaha yako ni ya muda tu, haitadumu. Uwe na uhakika kuwa atarudi kwa mtoto wake. Wewe kwake huna maana, mayai yenyewe uliyakausha kwa uzembe wako," ernesterina71 alimwambia Sepetu.

Sepetu hakuyatilia maanani maoni haya ila aliwaonya dhidi ya kuwatakia watu mabaya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved