Winnie Odinga amkumbuka marehemu ndugu yake

Ingekuwa siku yako ya kuzaliwa ya 49 leo. Pumzika Baba Alay," aliandika.

Muhtasari
  • Ujumbe huo ulishirikiwa pamoja na picha ya kaka mkubwa aliyevalia sare za shule na Winnie akiwa msichana mdogo
Winnie Odinga
Winnie Odinga

Binti ya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga Winnie alimkumbuka marehemu kaka yake Fidel Castro Odinga, miaka kadhaa baada ya kifo chake cha ghafla mnamo 2015.

Winnie ambaye ameonyesha nia ya siasa alisema anamkosa kaka yake ambaye alifariki katika mazingira yasiyoeleweka.

Fidel alichukuliwa kuwa mrithi wa kisiasa wa babake Odinga.

Wakati akichapisha picha kwenye stori zake za Instagram, Winnie ambaye baada ya uchaguzi alichukua muda kutoka kwenye mitandao ya kijamii, alisema leo ingekuwa ni siku ya kuzaliwa ya 49 ya Fidel.

Ujumbe huo ulishirikiwa pamoja na picha ya kaka mkubwa aliyevalia sare za shule na Winnie akiwa msichana mdogo.

 

Ingekuwa siku yako ya kuzaliwa ya 49 leo. Pumzika Baba Alay," aliandika.

Tangu kifo cha mzaliwa wa kwanza wa Raila, chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi licha ya uchunguzi kufanywa.