Diamond kusafirisha mashabiki wa soka hadi Qatar kutazama Kombe la Dunia

Diamond ametangaza ofa maalum kwa mashabiki wa kandanda wanaoweka dau kupitia Wasafi Bet.

Muhtasari

•Kampuni ya Ubashiri ya Wasafi Bet ilizindua promosheni ya Twende Qatar Na WasafiBet katika ukumbi wa Milimani City.

•Baba Levo alidokeza kuwa kadiri mtu anavyocheza mara nyingi zaidi ndivyo anavyoboresha nafasi yake ya kushinda.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Bosi wa Wasafi Media Diamond Platnumz ametangaza ofa maalum kwa mashabiki wa kandanda wanaoweka dau kupitia Wasafi Bet.

Jumatano jioni, Kampuni ya Ubashiri ya Wasafi Bet ilizindua promosheni ya Twende Qatar Na WasafiBet katika ukumbi wa Milimani City.

Promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na mkurugenzi wa kampuni, Diamond inatoa nafasi kwa washiriki kamari wanaoweka dau la zaidi yaTsh 2000 (Ksh100)  kujishindia tiketi ya ndege ya kwenda Qatar kushuhudia moja kwa moja mashindano ya kombe la dunia yatayofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

"Leo rasmi mkurugenzi wa wasafibet Bw Diamond Platnumz amefungua promosheni mpya iitwayo Twende Qatar na Wasafibet ambayo ukibashiri kwa 2000 tu unapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuwania tiketi ya kwenda Qatar," WasafiBet ilitangaza Jumatano kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Wengine waliokuwepo wakati wa uzinduzi huo ni pamoja na mamake Diamond Mama Dangote Zuchu, Baba Levo, Mwijaku, H-Baba, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James pamoja na wageni wengine wakuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, mmoja wa mabalozi wa WasafiBet, Baba Levo alifichua sheria na kanuni za promosheni hiyo.

"Ili uweze kushiriki, cha kwanza ujisajili na WasafiBet. Cha pili ubet mechi kuanzia tano kuendelea mbele. Cha tatu, hizo mechi ziwe na odds kuanzia 1.5. Cha tatu, mkeka wako uwe kuanzia 2000 kuendelea mbele," alisema.

Baba Levo alidokeza kuwa kadiri mtu anavyocheza mara nyingi zaidi ndivyo anavyoboresha nafasi yake ya kushinda.

Hapo awali, Diamond alikuwa amewaacha watu wakidhani kuwa ana nia ya kuzindua shirika la ndege baada ya kuchapisha picha ya ndege kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.