Sauti Sol wawafariji familia zilizowapoteza wapendwa wao baada ya ajali ya ndege

Waliandika kwamba mawazo na sala zao ziko kwa abiria waliojeruhiwa na wafanyikazi wa ndege.

Muhtasari
  • Sauto Sol wawafariji familia zilizowapoteza wapendwa wao baada ya ajali ya ndege

Huku watu wakizidi kuomboleza wapendwa wao baada ya ndege kuanguka ziwa Victoa siku ya jumapili asubuhi bendi ya Sauti Sol Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wao wa Instagram waliandika ujumbe wa rambirambi kwa  familia za waliopoteza wapendwa wao.

Waliandika kwamba mawazo na sala zao ziko kwa abiria waliojeruhiwa na wafanyikazi wa ndege.

Pia waliongeza kuwa wanawatakia ahueni ya haraka.

"Kwa mioyo ya majonzi, tunatoa pole kwa familia, marafiki na wafanyakazi wote waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya ndege ya Precision Air. Mawazo na sala zetu ziko pamoja na abiria waliojeruhiwa na wafanyakazi wa ndege. Tunawatakia wote afueni ya haraka."

Ndege hiyo ilianguka ziwa Victoria siku ya Jumapili asubuhi, huku ikisababisha vifo vya watu 19.