Jamaa aliyeshinda Ksh 20.8M alia baada ya mpenzi wake kutoroka na pesa hizo zote

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 49 walikuwa wameishi na mpenzi wake pamoja kama wanandoa kwa miaka 26.

Muhtasari

• Inaaminika mkewe alitoroka na pesa hizo huku duru za kuaminika zikisema kuwa warishirikiana na mpenzi wake mpya kutoroka na kima hicho cha fedhaa.

Image: Maktaba

Mwanamume mmoja nchini Thailand analia  kwa kukosa hata senti moja  baada ya mpenzi wake waliofunga ndoa naye kumwimbia pesa alizokuwa ameshinda kwenye mchezo wa bahati nasibu.

Mwanamume huyo, Manit mwenye umri wa miaka 49, alijawa na furaha baada ya kushinda takrima ya shilingi milioni 20.8 ambayo ni pauni 140,856 kwenye mchezo huo wa kamari.

Manit alisema kuwa walikuwa na mpango na mkewe Angkanarat, kutoa sehemu kidogo ya pesa hizo kwenye hekalu kama njia ya kutoa shukrani na kisha wafumukane wote na familia yake kufunga safari ya kwenda sherehe ya kufurahia ushindi wake.

Alizieka pesa hizo kwenye akaunti ya mkewe kwa hiari bila kujua mkewe alikuwa na mpango wa kando na mwanamume mwingine. Tangu wakati huo Mahit hajawahi wasiliana na Angkanarat.

Inaaminika mkewe alitoroka na pesa hizo huku duru za kuaminika zikisema kuwa warishirikiana na mpenzi wake mpya kutoroka na kima hicho cha fedhaa.

Manit alipigwa na butwaa wakati ambapo mtoto mmoja wa familia hiyo alifichua alikuwa anajua fika njama ya mama yao ya kuiba pesa hizo na pia alijua mama yao alikuwa ana mpenzi nje ya ndoa kisiri. Ila hakumwambia baba yake.

Polisi walisema  hawawezi kumsaidia Manit kwani yeye na Angkanarat hawakuwahi kutia sahihi cheti chochote cha ndoa, licha ya kuwa pamoja kwa miaka 26 na kujaliwa watoto 3.

Polisi walisema hakuna kitu wangeweza kufanya, ilionekana tu kwamba Manit alikuwa amemtumia pesa hizo mkewe kwa hiari na angelichokifanya ni kujaribu kumshawishi mkewe arudishe pesa hizo.

Hatimaye, Manit aligeukia vyombo vya habari vya Thailand katika jaribio la kuwasiliana na mkewe kuwa na mkono wa huruma na kurudisha pesa hizo za bahati yake.