Hisia mseto baada ya Jaymo Ule Msee kuwaonya wanaume kutumia hustler Funds kujiburudisha

Anasema kuwa pesa hizo zitakuwa msaada kwa wale walio katika biashara

Muhtasari
  • benvick2001: Wakenya Hio tutakula alafu tujisot badaye ni hustler's fund always hustling 😂😂😂
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Jaymo Ule Msee

Muunda maudhui na mchekeshaji Jaymo ule Msee amewashauri vijana wa kiume kuepuka kuchukua mkopo wa Hustler Fund ikiwa una nia ya kufanya sherehe na pesa hizo.

Anasema kuwa pesa hizo zitakuwa msaada kwa wale walio katika biashara na wale walio na mawazo mazuri ya biashara.

"Tafadhali Msichukue Hustler Fund halafu mtume Kama Fare ama Favours Kwa watu...Hio pesa ni ya biashara sio kufurahia!!!Kumbuka serikali iko na mkono mrefu kuliko yako 😂😂,"Alisema Jaymo.

Wanamitandao na mashabiki walitoa hisia mseto, na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

benvick2001: Wakenya Hio tutakula alafu tujisot badaye ni hustler's fund always hustling 😂😂😂

Kennedy Mc Oloto: Which kind of business can you start with 475= in Kenya nowadays?

Mc Rack KE: Jaymo alikua was tiiiigisha mti 😹 arelax next ,,, tutigike 😹I heard one netizen saying ,,,

Jose Tu: Mnatutupea pesa ya chrome nusu na mnaanza kuleta masharti..nkt!!😅😅

Moureen Kithome: This information would have been more useful if you posted it early morning but saa hii saa name tumekunywa chrome pyu

Morgan De Dutch: Wacha waendelee kuongoea Kenya kuna vitu mingi za kutishiwa Hustler fund to be added in the list, Mimi nishachukua zangu nipige sherehe legit niende vacation Mombasa nkimaliza mtu anionyeshe jela yenye nitafungwa 😹😹😹