Ommy Dimpoz , Idris Sultan wamuomboleza aliyekuwa mpenzi wao Maya Mia

Ripoti zinaashiria kuwa marehemu Maya Mia alijitoa uhai.

Muhtasari

•Mfanyibiashara wa vipodozi wa Tanzania na Macedonia Maya Mia ameaga dunia baada ya kudaiwa kujitoa uhai.

•“R.I.P mpenzi wangu,” Dimpoz alisema na kuambatanisha ujumbe wake na emoji inayoashiria kuvunjwa moyo.

Mfanyibiashara wa vipodozi wa Tanzania na Macedonia Maya Mia ameaga dunia baada ya kudaiwa kujitoa uhai.

Mia aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchekeshaji/mwigizaji wa Tanzania Idris Sultan na mwimbaji Ommy Dimpoz, lakini kwa nyakati tofauti.

Marehemu alichumbaiana na Idris Sultan mwaka wa 2018 na akawa na uhusiano na Ommy Dimpoz mwaka wa 2020.

Mia alizaliwa Makedonia lakini alikuwa ameishi Tanzania kwa zaidi ya mwongo  mmoja. Ripoti zinaashiria kuwa kabla ya kifo chake, alikuwa akiishi Afrika Kusini.

Ommy Dimpoz alithibitisha kifo cha mpenzi huyo wake wa zamani na kumwomboleza. Kama njia ya kumwomboleza mlimbwende huyo, Dimpoz alichapisha picha kadhaa za kumbukumbu zao.

“R.I.P mpenzi wangu,” alisema na kuambatanisha ujumbe wake na emoji inayoashiria kuvunjwa moyo.

Pia alibadilisha picha yake ya  Instagram na kuweka selfie yake na marehemu Maya wakiwa pamoja.

Huku akimuomboleza mpenziwe wa zamani, Idriss Sultan alichapisha video ya kumbukumbu zake maalum na kipusa huyo.

"💔 … Innalillahi wainna illaihi rajighun 🙈" ((Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)." aliandika chini ya video hiyo.

Mamia ya watumiaji wa mtandao pia waliomboleza malkia huyo mrembo mzaliwa wa Macedonia chini ya machapisho yake ya hivi majuzi ya Instagram.

@mr_kukutuz Jamani umeondoka umeniacha na majonzi

@chief_njapuka Daah 😥😥😥 Maya umejua kuniweza

@officialaine3 Najua uko kwenye mioyo yetu ukituangalia na kutuelekeza. Tunakumiss sana. Pumzika kwa amani Maya.

@s.aziz Nimevunjika dada

bbjaylisa24x Mbona umetuacha kaka zetu walia huku, rudi banaa