Tanzia! Muigizaji mkongwe Gibson Gathu 'Prosecutor' ameaga dunia

Gathu alifanyiwa upandikizi wa figo mwezi Julai.

Muhtasari

•Gathu anaripotiwa kufariki katika hospitali ya Mediheal, mjini Eldoret ambako alikuwa akipokea matibabu.

•Gathu alikuwa akipambana na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miongo miwili.

Mwigizahi wa Vioja Mahakamani Gibson Gathu
Mwigizahi wa Vioja Mahakamani Gibson Gathu
Image: HISANI

Muigizaji mkongwe Gibson Gathu Mbugua ameaga dunia.

Gathu ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na uhusika wake katika kipindi cha Vioja Mahakamani kwenye KBC anaripotiwa kufariki Alhamisi asubuhi katika hospitali ya Mediheal, mjini Eldoret ambako alikuwa akipokea matibabu.Marehemu aliigiza kama 'Prosecutor' (Kiongozi wa Mashtaka) katika Vioja Mahakamani.

Takriban miezi mitano iliyopita muigizaji huyo gwiji alifanyiwa upandikizi wa figo katika hospitali ya Mediheal baada ya Wakenya kumfanyia mchango. Rais wa zamani Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa waliochangia matibabu yake huku akitoa milioni mbili.

Aliruhusiwa kuenda nyumbani mwezi Agosti ambapo alithibitisha kwamba alikuwa akijisikia nafuu na mwenye nguvu baada ya upasuaji huo.Hali yake hata hivyo ilidhoofika na akakimbizwa katika hospitali hiyo ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hadi alipoaga dunia siku ya Alhamisi asubuhi.

Mwezi Aprili, Gathu alitoa wito kwa wasamaria wema kumsaidia kuchangisha Ksh6 milioni kwa ajili ya matibabu ya figo.

Gathu alikuwa akipambana na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miongo miwili.

Familia yake imesema matibabu yake yamewasababisha matatizo ya kifedha na hivyo wanahitaji kusaidiwa kuchanga pesa za kugharamia upasuaji utakaofanyika Julai 22, 2022.

"Gib amekuwa akipambana na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miaka 20. Mwezi Novemba 2020m figo zake zilikosa kufanya kazi na amekuwa akienda kupokea matibabu ya dialysis mara mbili kwa wiki. Hii imesababisha shida za fedha katika familia," Tangazo lililofikia Radio Jambo lilisoma.

Familia ya muigizaji huyo imesema kwamba tayari amepata mtu wa kumtolea figo moja. Wamesema kuwa fedha wanazoziomba zinajumuisha gharama za upasuaji na ma