Skendo kubwa zilizowahusisha Wakenya mashuhuri 2022

Kumekuwa na mambo mengi mazuri na mabaya mwaka mzima.

Muhtasari

•Kumekuwa na skendo kadhaa zinazohusisha baadhi ya Wakenya mashuhuri katika nyakati tofauti za mwaka wa 2022.

Karen Nyamu, Samidoh, Diana Marua, Size 8, DJ Mo
Image: HISANI

Mwaka wa 2022 umekuwa mwaka mkubwa katika sekta ya burudani ya Kenya, kumekuwa na mambo mengi mazuri na mabaya mwaka mzima.

Kama kawaida, kumekuwa na skendo kadhaa zinazohusisha baadhi ya Wakenya mashuhuri katika nyakati tofauti za mwaka wa 2022.

Tunapouaga mwaka wa 2022, tumeangazia baadhi ya skendo kubwa zilizoshuhudiwa nchini Kenya mwaka huu.

1. SAMIDOH NA KAREN NYAMU

Skendp kubwa zaidi kushudiwa katika siku za hivi majuzi iliwahusisha senata wa kuteuliwa Karen Nyamu, mzazi mwenza wake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh na mkewe Samidoh Edday Nderitu.

Watatu hao walihusika katika vita wakati wa shoo ya Samidoh iliyofanyika siku chache zilizopita jijini Dubai. Matukio hayo yalinaswa kwenye video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuzungumziwa sana na Wakenya.

Seneta Nyamu pia alirekodiwa akizua drama na kufurushwa kutoka kwenye jukwaa ambapo Samidoh alikuwa amesimama.

Baada ya matukio hayo, Nyamu alitangaza kukatiza mahusiano yake na staa huyo wa Mugithi na akaapa kuangazia kazi yake ya useneta.

2. MARY LINCOLN

Mwimbaji Mary Lincoln akiombewa kanisani
Image: FACEBOOK// MARY LINCOLN

PIcha ya uchi ya mwimbaji wa nyimbo za injili Mary Lincoln ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii mwezi Novemba, 2022.

Mwanamuziki huyo ambaye alionekana kujuta yaliyompata baadae alijitokeza kukiri kosa lake, kutubu na kuomba msamaha

Pia aliachia wimbo wa injili ambapo aliangazia skendo hiyo.

3. SAMMY IRUNGU

Mwimbaji mwingine wa nyimbo za injili za Kikuyu Sammy Irungu pia alikuwa mwathiriwa wa picha za uchi ambapo video zake zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo mwezi Novemba, 2022.

Irungu baadae alijitokeza na kuvunja kimya kuhusu video hiyo huku akimshtumu shetani kwa masaibu yaliyomkumba.

4. SIZE 8 NA DJ MO

Wanandoa Size 8 na mumewe DJ Mo wanasemekana kuvunja ndoa yao
Wanandoa Size 8 na mumewe DJ Mo wanasemekana kuvunja ndoa yao
Image: MpASHO

Wanandoa mashuhuri Size 8 na DJ Moh walikuwa wamekatiza ndoa yao kwa muda mwishoni mwa mwezi Agosti, 2022.

Size 8 ambaye ni mwimbaji wa injili aliripotiwa kugura ndoa yake na kuwachukua watoto wao baada ya penzi lake na Mo kuyumba.

Wawili hao hata hivyo walisuluhisha mzozo wao kwa usaidizi wa viongozi wa kanis na kurudiana siku chache baadae.

5.SIMON KABU NA SARAH KABU

Mapema mwaka uliopita, wanandoa Simon Kabu na Sarah Kabu pia walikuwa wamevunja ndoa yao kwa muda na kwenda njia tofauti.

Mnamo mwezi Aprili 2022  Bi Sarah alikiri kwamba ndoa yao haikuwa ikiendelea sawa kwa muda na kudokeza mipango ya talaka.

Sarah Kabu na Simon Kabu
Sarah Kabu na Simon Kabu
Image: HISANI

Sarah alikiri alikuwa akijua kuhusu watoto wengine wawili wa mumewe ambao alipata kutoka kwa mahusiano yake ya awali. Alieleza kuwa hata hivyo mahusiano ya zamani ya mumewe yalikuwa yakitikisa ndoa yao.

Baadae hata hivyo wanandoa hao waliweza kusuluhisha tofauti zao na kuendelea kuishi vizuri kama mume na mke.

6. DIANA MARUA

Mwezi Novemba 2022, video ya zamani ya mke wa mwimbaji Bahati, Diana Marua akikiri jinsi alivyokuwa akichumbiana na wanaume wengi iliibuka kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, Diana alizungumzia jinsi wanaume tofauti walivyokuwa wakikidhi mahitaji yake ya kifedha na kwa kurudisha shukrani angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao.

Wakenya walizungumza kuhusu video hiyo kwa zaidi ya wiki moja huku baadhi yao wakimshinikiza Bahati kusitisha uhusiano na mama huyo wa watoto watatu.