logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kujisalimisha sio amri, ni aina ya hekima inayojulikana tu na mke wa mtu - Amber Ray

"Ni utambuzi wa masafa ya juu ambayo yanaweza kukubadilisha kuwa taswira bora yako mwenyewe."

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 January 2023 - 10:11

Muhtasari


  • • Amber Ray alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Kennedy Rapudo mwishoni mwa mwaka jana.
  • • Wawili hao pia walitangaza kutarajia mtoto pamoja.
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray

Mwanamitindo Amber Ray tangu avishwe pete ya uchumba na Kennedy Rapudo, amekuwa akiweka maneno yake kwenye mizani kabla ya kuyatamka, kinyume na hapo awali ambapo alikuwa anabwabwaja tu bila kujali nani anafikiwa na maneno hayo.

Ray alivishwa pete ya uchumba mwishoni mwa mwaka jana wakiwa ziarani Dubai na kwa sasa ni bibi harusi mtarajiwa iwapo kila itu kitaenda sawa.

Tayari yeye na mchumba wake Rapudo wameshatangaza kutarajia mtoto pamoja na Ray amemsifia mwanamume huyo kwa kumpa heshima kwa wanawake wengine alipomvisha pete hadharani machoni pa marafiki na watezi wake.

Amber Ray sasa anatoa ushauri uliokolea munyu kwa wanawake wengine kuhusu kujisalimisha kwa mwanamume wako.

Kulingana naye, kujisalimisha hakukufanyi kuwa dhaifu wala kuonekana mtumwa bali ni njia ya kudhihirisha busara uliyo nayo kwa mwanamume wako.

Mwanamitindo huyo alitoa tofauti na kufafanua kati ya kujisalimisha kwa mtu na kumtii mtu, huku akisema kuwa kujisalimisha si kitendo  bali ni utambuzi wa taswira yako mbele ya mwanamume wako.

“Kujisalimisha sio utii! Utiifu ni kufuata mawazo na hauna matumizi madogo kwa akili. Kujisalimisha sio kitendo! Ni utambuzi wa masafa ya juu ambayo yanaweza kukubadilisha kuwa taswira bora yako mwenyewe. Kujisalimisha sio amri, ni aina ya hekima inayojulikana tu na mke wa mtu mwenye maono makubwa. Ni uwanja uliowekwa na mwanaume kwa mwanamke kupumzika na kufurahia maisha,” Amber Ray alisema.

Walionekana pamoja na Rapudo wakila bata nono katika mgahawa mmoja wa kifahari, huku nyuso zao zikiwa zimeng’aa kwa tabasamu angavu.

Bilas haka kwa ushauri huu, taswira ya Ray kwa wengi itakuwa inabadilika kutoka kwa kuonekana kama mtu wa kujishaua mitandaoni na kutoka kimapenzi na wanaume wa watu hadi kuwa mwanamke aliyetulia katika ndoa na mume wake halali.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved