Mikopo ya mamilioni ya fedha kwa wasanii Tanzania yazua mjadala

Serikali ya Tz imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya karibu bilioni 1 kwa wasanii.

Muhtasari

•Fedha hizo zimetolewa kwa awamu mbili zikihusisha wasanii wa sanaa na utamaduni waliokidhi vigezo.

•Wanaounga mkono wanasema ni hatua muhimu ya kukuza sanaa ya Tanzania.

Image: BBC

Serikali ya Tanzania kupitia mfuko wa utamaduni ulio chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya karibu bilioni 1 kwa wasanii wa nchi hiyo.

Fedha hizo zimetolewa kwa awamu mbili zikihusisha wasanii wa sanaa na utamaduni waliokidhi vigezo ikiwemo usajili na urasimishaji wa Kazi za sanaa na utamaduni ambapo kilikuwa moja ya kigezo kwenye kupata mkopo huo.

Hata hivyo hatua hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti wapo wanaaona wangestahili kupewa wasanii wachanga zaidi ili kuwawezdesha kukuwa kuliko kupewa magwiji wa sanaa na wenye majina ambao tayari walishakomaa kwenye sanaa.

Abdul Nondo, kiongozi wa vijana wa chama cha ACT Wazalendo yeye anasema kama serikali ina uwezo wa kutoa mikopo kwa wasanii ifanye hivyo kwa kuwaongezea mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu wenye mahitaji makubwa ya mikopo.

twitterRipotiReport this social embed, make a complaint

Hili likaungwa mkono na Brisco Mkottery Jr aliyeonyesha kwenye mtandao wake wa twitter kwamba inastahili kwenda kwa wanafunzi vyuoni.

twitterRipotiReport this social embed, make a complaint

Wanaounga mkono wanasema ni hatua muhimu ya kukuza sanaa ya Tanzania.

Hundi za fedha hizo zilikabidhiwa na waziri wa wizara hiyo Mohamed Mchengerwa na kuhudhuriwa na viongozi wengine akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Nyakaho Mturi Mahemba.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi hizo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sana, Mahemba aliseme: "Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ulianzishwa kwa lengo la kuwezesha tasnia ya sanaa kujiendesha yenyewe na unatoa Huduma za mafunzo na mikopo ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya sanaa kujikwamua kiuchumi".

Juni mwaka jana akiwa bungeni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa alisema serikali ilisema inakusudia kuanza kutoa mikopo nafuu kwa wasanii 500 wa utamaduni na sanaa kupitia mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania katika mwaka wa fedha 2022/23.

Miongoni mwa wasanii wakubwa walipata mikopo hiyo ya awamu ya pili jana inayofikia 850mil ni Jacob Stephen(JB), Iren Uwoya, Ray Kigosi, DJ Ally B, Mzee Yusuph, Jacquiline Wolper, Chiba Kismati na Rutasingwa Bushoke.