Rihanna afichua ujauzito katika kipindi cha mapumziko cha Super Bowl

Wawakilishi wake walithibitisha kuwa mwimbaji huyo alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Muhtasari

•Ingawa baadhi ya mashabiki walikiri kusikitishwa na kwamba hii itamaanisha kuchelewa tena kwa albamu ya tisa ya Rihanna, mapokezi kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa ya furaha sana.

Image: INSTAGRAM// RIHANNA

Rihanna alitoa shoo ya kusisimua na habari ambazo wengi hawakutarajia wakati wa mapumziko kwenye Super Bowl ya Jumapili, lakini mitandao ya kijamii ilijawa na mengi kuhusu hatua ya mwimbaji huyo kufichua mgeni maalum ambaye hakutarajiwa.

Katika mahojiano wiki iliyopita, Rihanna aliulizwa kama kutakuwa na mambo ya kushangaza wakati wa onyesho lake kwenye Uwanja Arizona's State Farm Arizona.

"Nafikiria kumleta mtu,"mwimbaji wa Bajan alijibu."Sina hakika, tutaona."

Kwa kawaida, mashabiki walidhani kwamba alikuwa akizungumza kuhusu mmoja wa wasanii wengi ambao alishirikiana nao wakati wa kazi yake ya sanaa.

Lakini Rihanna hakuwa akimaanisha yeyote kati yao na alikuwa akidokeza kwamba alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Ndani ya saa moja baada ya onyesho la Rihanna kufikia tamati, huku mashabiki wake wakijadiliana kuhusu muda gani ujauzito wake umedumu wawakilishi wake walithibitisha kuwa mwimbaji huyo alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Ingawa baadhi ya mashabiki walikiri kusikitishwa na kwamba hii itamaanisha kuchelewa tena kwa albamu ya tisa ya Rihanna, mapokezi kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa ya furaha sana.